Unju bin Unuq : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 19:
 
==Asili ya jina la Unju bin Unuq katika Uarabuni na Biblia==
Jina lake latokana na Kiarabu ‘Uj bin Unuq / ‘Anaq <big>عوج بن عنق</big> anayejulikana katika visa vya nchi nyingi za Uislamu kama jitu mkubwa sana. Waislamu walipokea hadithi kutoka Wayahudi anakojulikana kwa jina la Og <big>עוֹג‬</big>.
 
Asili kabisa ni taarifa kuhusu mapigano kati ya Wanaisraeli waliotoka Misri na Ogu mfalme wa Bashani (Hesabu 21,33)<ref>Bashani ilikuwa eneo katika Syria ya leo, upande wa kusini ya Dameski.</ref>; Wanaisraeli walimshinda wakiongozwa na Musa. Ogu alisemekana kuwa mtu mrefu; [[Kumbukumbu ya Torati]] 3,11 inamtaja hivi: "aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda,na upana wake mikono minne,kwa mfano wa mkono wa mtu". Katika masimulizi ya Wayahudi tabia hii iliendelea kuongezeka; katika Amosi 2,9 anatajwa (bila kusema jina) kama "Mwamori" "nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni". Wataalamu Wayahudi wa baadaye waliona ya kwamba vipimo vya Kumb. 3 kuhusu kitanda chake chenye urefu wa mikono yaani [[dhiraa]] 10 sawa na mita 4-5 vilihusu mkono wa huyu jitu mwenyewe hivyo walimwona mkubwa zaidi tena. Kwenye kitabu Berakhot cha [[Talmudi]] Ogu anasiimuliwa ya kwamba aliweza kuinua mlima aliotaka kurusha dhidi ya Wanaisraeli lakini Mungu alimzuia<ref>[http://www.halakhah.com/berakoth/berakoth_54.html#chapter_ix Berakhot 54b], Babylonian Talmud: Tractate Berakoth </ref> Katika kitabu cha Nidah katika Talmudi Ogu anasemekana ni mtu aliyeishi kabla ya gharika ya Nuhu akiwa ni mmoja wa hao ambao walitunzwa.<ref>[http://www.halakhah.com/pdf/taharoth/Nidah.pdf Talmud - Mas. Nidah 61a],English Babylonian Talmud, SEDER TOHOROTH, tractate Nida </ref>
 
Masimulizi ya Kiyahudi yalipokelewa na Waislamu na kubadilishwa tena. Ushahidi uko kwa [[Al Tabari]] aliyeandika ya kwamba maiti ya Udj ilikuwa kama daraja juu ya [[mto Naili]], pia wengine.<ref>Angalia makala UDJ katika Encyclopedia of Islam, uk. 777</ref>
 
 
 
==Tanbihi==