Historia ya Iceland : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''{{PAGENAME}}''' inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Iceland. {{Europe topic|Historia ya}} {{mbegu-historia}} Jamii:Historia ya Icela...'
 
No edit summary
Mstari 1:
'''{{PAGENAME}}''' inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda [[Jamhuri]] ya [[Iceland]].
 
== Historia ya awali==
Iceland iko mbali na [[bara]] la [[Ulaya]] na la [[Amerika]] tena katika [[mazingira]] ya [[baridi]]. Hivyo inaaminika haikuwa na [[watu]] kabisa hadi mwaka [[800]] [[BK]]. [[Wataalamu]] hawakubaliani kama ni ma[[baharia]] kutoka [[Norwei]] au [[Eire]] waliobahatika kufika [[Kisiwa|kisiwani]] na kujenga makao ya kwanza.
 
Hakika waliofika wengi kidogo walikuwa [[Waviking]] au Wa[[norwei]] wa kale katika [[karne ya 9]]. Kama Waeire walikuwepo walifukuzwa au kuwa sehemu za Waviking. Mtu wa kwanza aliyekumbukwa kwa [[jina]] alikuwa [[Flóki Vilgerðarson]].
 
Waviking waliofika walikuja pamoja na [[familia]] na [[watumishi]] au [[watumwa]] wao. Mnamo mwaka [[930]] ma[[chifu]] na wasimamizi wa familia zilizokuwepo walipatana kuhusu aina ya [[katiba]] kwa Iceland. Walianzisha [[bunge]] la [[Althing]]. Ulikuwa mkutano wa watu 36 walioitwa "Godi" wakiwa na [[cheo]] cha kuunganisha [[madaraka]] ya [[chifu]], [[hakimu]] na [[kuhani]]. Utaratibu huu wa kuwa na bunge umeendelea hadi leo bila kusimama. Hivyo Iceland ni nchi ya pekee ambako utaratibu wa ki[[demokrasia]] wa kale umeendelea wakati katika nchi za Ulaya nafasi ya [[wafalme]] au [[watawala]] wengine iliongezeka na kumeza [[haki]] zote za watu wa kawaida.
 
Mwaka [[985]] Mwiceland aligundua njia ya kufika [[Greenland]] na baadaye [[Amerika ya Kaskazini]]. Mviking "[[Erik Mwekundu]]" alifukuzwa kisiwani kwa sababu alikuwa [[mwuaji]]. Alielekea [[magharibi]] kwa [[jahazi]] yake na kufika kwanza Greenland halafu [[pwani]] ya [[Kanada]] ya leo. Aliita bara jipya "nchi ya [[mzabibu]]" kwa sababu alikuta aina ya mizabibu isipokuwa bila ma[[tunda]].
 
==Chini ya Norwei na Denmark==
Tangu [[1262]] uhuru wa Iceland ulikwisha kwa sababu viongozi walijiunga na [[Ufalme wa Norwei]]. Iceland iliendelea kuwa na bunge lake na madaraka mbalimbali - hasa kwa sababu [[usafiri]] uliendelea kuwa mgumu - lakini mabwana wakuu walikuwa sasa wafalme wa [[Skandinavia]], kwanza Wanorwei, baadaye Wa[[denmark]].
 
Mwaka [[1918]] [[Denmark]] ilirudisha madaraka yote ya [[serikali]] kwa Waiceland wenyewe isipokuwa mfalme wa Denmark aliendelea kama Mkuu wa nchi.
 
Wakati wa [[Vita Kuu ya Dunia ya Pili]] Denmark ilivamiwa na [[Ujerumani]] na Althing iliamua ya kwamba kuanzia sasa kisiwa kitajitawala kabisa. Mwaka [[1944]] Iceland ilipata [[uhuru]] kamili.
 
Baada ya [[vita]] kwisha Iceland ilipata kuwa nchi mwanachama ya [[NATO]] lakini haina [[wanajeshi]] hadi leo. Ilifanya [[mkataba]] na [[Marekani]] ya kuwa Wamarekani wanapewa [[haki]] ya kutumia kituo cha [[Ndege (uanahewa)|ndege]] kisiwani na kwa upande mwingine wanaahidi kutetea Iceland.
 
{{Europe topic|Historia ya}}