Unju bin Unuq : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Muhammad ibn Muhammad Shakir Ruzmah-'i Nathani - The Demon 'Uj ibn 'Unuq Carries a Mountain with which to Kill Moses and His Men - Walters W659143B - Full Page.jpg|thumb|350px|Unju bin Unuq akibeba mlima anaotaka kurusha dhidi ya Musa; picha katika nakala ya [[Kituruki]] ya Kitabu ''‘Ajā’ib al-makhlūqāt'' (maajabu ya viumbe) كتاب عجائب المخلوقات وغرائب الموجودات cha Zakarīyā’ ibn Muḥammad al-Qazwīnī]]
[[Picha:The tallest man in the world, Sultan Kosen (4046630148).jpg|alt=Mtu mrefu huko iceland|thumb|[[Mtu]] mrefu kuliko wote [[duniani]] alipotembelea [[Iceland]].]]
'''Unju bin Unuq''' (pia: '''Unju bin Unuku''', '''Unzi Bin Ununuk''') ni [[jina]] la [[jitu]] katika masimulizi ya wakazi wa [[pwani]] ya [[Tanzania]]. [[Hadithi]] zake zasimuliwa kuanzia [[Bagamoyo]] hadi [[Kilwa]].
 
Mstari 17:
 
==Asili ya jina la Unju bin Unuq katika Uarabuni na Biblia==
[[Jina]] lake linatokana na [[Kiarabu]] ‘Uj<sup>c</sup>Udj bin Unuq / ‘Anaq <big>عوج بن عنق</big> anayejulikana katika visa vya nchi nyingi za [[Uislamu]] kama jitu kubwa sana. Waislamu walipokea [[hadithi]] kutoka kwa [[Wayahudi]] anakojulikana kwa jina la Og <big>עוֹג‬</big>.
 
[[Asili]] kabisa ni taarifa za Biblia kuhusu mapigano kati ya [[Wanaisraeli]] waliotoka [[Misri]] na [[Ogu]] [[mfalme]] wa [[Bashani]] ([[Hesabu (Biblia)|Hesabu]] 21,33)<ref>. Bashani ilikuwa eneo la [[Syria]] ya leo, upande wa [[kusini]] wa [[Dameski]].</ref>; Wanaisraeli walimshinda wakiongozwa na [[Musa]].
Mstari 29:
Kwenye [[kitabu]] Berakhot cha [[Talmudi]] Ogu anasimuliwa ya kwamba aliweza kuinua [[mlima]] aliotaka kurusha dhidi ya Wanaisraeli, lakini [[Mungu]] alimzuia<ref>[http://www.halakhah.com/berakoth/berakoth_54.html#chapter_ix Berakhot 54b], Babylonian Talmud: Tractate Berakoth </ref>. Katika kitabu cha Nidah katika Talmudi Ogu anasemekana ni mtu aliyeishi kabla ya [[gharika]] ya [[Nuhu]] akiwa ni mmoja wa hao ambao walitunzwa.<ref>[http://www.halakhah.com/pdf/taharoth/Nidah.pdf Talmud - Mas. Nidah 61a],English Babylonian Talmud, SEDER TOHOROTH, tractate Nida </ref>
 
==Katika Uislamu==
Masimulizi ya Kiyahudi yalipokewa na Waislamu na kubadilishwakupanushwa tena. Ushahidi uko kwa [[Al Tabari]] aliyeandika ya kwamba [[maiti]] ya <sup>c</sup>Udj ilikuwa kama [[daraja]] juu ya [[mto Naili]], pia wengine.<ref>Angalia makala UDJ katika Encyclopedia of Islam, uk. 777</ref>
 
Al-Tha<sup>c</sup>labi aliandika ya kwamba <sup>c</sup>Udj alikuwa na urefu wa dhiraa 23,333 akiweza kunywa kwenye mawingu, kushika ngumi baharini na kuichoma kwenye Jua. Alitembea mbele ya Nuhu wakati wa gharika kuu lakini maji yalifikia magoti yake tu. Aliishi miaka 36,000. Alipoona kambi la Wanaisraeli na Musa alivunja mlima akashika kipande cha kuangamiza kambi lote kwa pigo moja lakini Mungu alituma ndege waliokula shimo katikati ya mlima uliomangukia na kumfunga katikati. Hivi Musa aliweza kumshinda kirahisi.<ref>Angalia makala <sup>c</sup>UDJ katika Encyclopedia of Islam, uk. 777</ref>
 
==Tazama pia==