Nyota nova : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Nyota nova''' (lat. ''stella nova'' kwa maana ya "'''nyota mpya'''", ing. ''nova'') ni ongezeko la ghafla la mwangaza unaoonekana|mwangaza...'
 
No edit summary
Mstari 1:
'''Nyota nova''' ([[lat.]] ''stella nova'' kwa maana ya "'''nyota mpya'''", ing. ''[[:en:nova|nova]]'') ni ongezeko la ghafla la [[mwangaza unaoonekana|mwangaza]] wa nyota. Ilhali idadi kubwa za nyota hazionekani kwa macho matupu ongezeko hili linatokea mara nyingi kama "nyota mpya" angani inayoweza kung'aa sana hata kushinda nyota zote nyingine. Hivyo inaonekana kwa muda tu ikipotea baadaye tena kwa mtazamaji asiye na darubini.
 
==Historia ya utazamaji==
Mstari 6:
Lakini kuna taarifa za kale kuhusu nyota mpya zilizotokea angani na ile ya kale zaidi ni ya wanaastronomia Wachina wa mwaka 185 kuhu nyota geni iliyoonekana karibu na [[Rijili Kantori|Rijili Kantori ''(α Centauri)'']]. Nova nyingine ilitazamiwa mwaka 1006 na kurekodiwa na wanaastronomia Wachina, Wajapani na Wakristo wa Baghdad, mabaki yake huonekana hadi leo kama "Nebula ya Kaa" katika eneo la [[Tauri (kundinyota)|Tauri ''(Taurus)'']].
 
==Tofauti kati ya Nova na Supanova==
Tangu katikati ya karne ya 20 vipimo vilileta wanaastronomia kutofautisha kati ya "nova" na "supanova" ambazo zote ni "nyota mpya" zinazotokea angani kwa muda lakini kwa sababu tofauti. Nova ya Tycho Brahe sawa na nova ya mwaka 1006 siku hizi zinaitwa "supanova" maana zilikuwa milipuko ya nyota zilizoharibika kutokana na matukio haya. Neno "nova" linataja sasa kuwaka kwa muda kwa nyota katika [[nyota pacha|mfumo wa nyota pacha]] inyoendelea kuonekana baadaye kama kabla ya kuwaka.
Tangu katikati ya karne ya 20 vipimo vilileta wanaastronomia kutofautisha kati ya "nova" na "supanova" ambazo zote ni "nyota mpya" zinazotokea angani kwa muda lakini kwa sababu tofauti.
*Nova ya Tycho Brahe sawa na ile ya mwaka 1006 siku hizi zinaitwa "supanova" maana zilikuwa milipuko ya nyota zilizoharibika kutokana na matukio haya. Inayobaki ni wingu la mata yake iliyosambaa katika eneo kubwa kama Nebula ya Kaa.
 
*Neno "nova" linataja sasa kuwaka kwa muda kwa nyota ndani ya [[nyota pacha|mfumo wa nyota pacha]]. Katika hali ya nova nyota inaongeza mwangaza ghafla mara elfu kadhaa ya kawaida yake hadi kurudi tena baada ya wiki au miezi katika hali yake kama kabla ya kuwaka.
 
 
==Tabia za nova==
Nyota nova za kawaida zinatokea katika [[Nyota pacha|mfumo wa nyota pacha]]. Nadharia inayokubalika na wengi inasema: [[nyota kibete cheupe]] na nyota kubwa, hasa [[jitu jekundu]], zinazungukana kwa umbali wa karibu. Kibete cheupe kimeshamaliza hidrojeni yake na kujikaza, hivyo graviti yake bado ni kubwa ingawa mjao wake ni mdogo, pia ni joto sana. Jitu jekundu la jirani linaendelea kupanuka. Hapa sehemu ya mata ya matabaka za nje ya nyota kubwa inavutwa na graviti ya nyota ndogo na kuhamia upande wake. Sehemu ya mata hii ni hidrojeni inayokusanyika kwenye uso wa Kibete Cheupe kama namna ya angahewa. Hidrojeni hii inapashwa moto na uso wa Kibete Cheupe hadi kufikia halijoto ya kutosha ya kuanzisha [[myeyungano wa kinyuklia]] ''(nuclear fusion)''. Mchakato huu unaachisha kiasi kikubwa cha nishati inayorusha sehemu ya hidrojeni inayowaka kwenye anga la nje. Hii inaongeza mwangaza wa nyota inayoonekana sasa kama nyota nova.
(inaendelea)
 
Maendeleo ya nova inafuata hatua kama hizi:
* wakati myeyungano wa kinyuklia unaanza usoni mwa Kibete Cheupe mwangaza wake unaongezeka takriban [[mag]] 9 katika kipindi cha siku chache.
* mara nyingi mwangaza unabaki palepale kwa siku kadhaa; hatua hii haikutazamiwa kwa kila nova
* baada ya siku hadi wiki kadhaa mwangaza unaongezeka tena mnamo mag 2.
* kutoka kilele hiki mwangaza unaanza kupungua mnamo mag 3.5
* katika hatua inayofuata kuna kupoa tena, manmo mag 3, atika muda wa miezi hadi miaka kadhaa
* katika miaka au miongo inayofuata mwangaza unaendelea kupungua hadi kufikia tena hali ya awali.
 
Kinadharia mchakato huu unaweza kurudia mara kadhaa kwa sababu baada ya mlipuko wa angahewa ya nyota ndogo mata kutoka jirani mkubwa inaanza kuvutwa tena. Nyota RS Ophiuchi katika [[Hawaa (kundinyota)|kundinyota ya Hawaa]] ilitazamiwa kuwaka mara sita<ref>[https://www.aanda.org/articles/aa/full_html/2009/15/aa11417-08/aa11417-08.html Brandi, E.; Quiroga, C.; Mikołajewska, J. (2009). "Spectroscopic orbits and variations of RS Ophiuchi". Astronomy and Astrophysics. 497]</ref>: 1898, 1933, 1958, 1967, 1985 na 2006.
 
==Tanbihi==
<references/>
 
[[Jamii:Nyota]]