Uchimbaji madini : Tofauti kati ya masahihisho

uchimbaji wa madini ya thamani au nyenzo nyingine za kijiolojia kutoka duniani
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Uchimbaji madini''' ni kitendo cha kulima au kuchimba ardhi kwa ajiri ya kupata '''madini'''.Kitu chochote ambacho hakiwezi kukuzwa au kuundwa...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 13:54, 26 Februari 2018

Uchimbaji madini ni kitendo cha kulima au kuchimba ardhi kwa ajiri ya kupata madini.Kitu chochote ambacho hakiwezi kukuzwa au kuundwa lazima kichimbwe.Kile kitendo cha kuchukua madini kutoka ardhini ndicho kinaitwa uchimbaji madini.Uchimbaji madini unaweza kufanywa ili kupata madini ya kimetali au yasiyo ya kimetali mfano,Almasi,Dhahabu,Shaba,Makaa ya mawe,Chumvi,Chuma na hata gesi asilia.

Mchimbaji madini na mashine ya kuchimbia

.

Uchimbaji mwingine hufanywa kwa kuondoa uchafu juu ya ardhi.Uchimbaji huu huitwa uchimbaji wa juu ya ardhi.Uchimbaji mwingine hufanywa kwa kuchimba ndani zaidi kwenye ardhi kwenye mashimo ya machimbo ya madini.Aina hii ya uchimbaji huitwa ujimbaji wa ardhini.Lakini kuna baadhi ya madini yanachimbwa kwa njia tofauti kabisa na aina hizi za uchimbaji, mfano machimbo ya madini ya dhahabu. Mfanyakazi anyechimba madini huitwa mchimba madini.Uchimbaji wa madini chini wa chini ya ardhi ni wa hatari sana,wachimba madini kila mwaka hufa kwenye ajari hizo .Mara nyingi katika nchi maskini.kifaa muhimu kwa ajiri ya kuongeza usalama hutumika ili kupunguza ongezeko la vifo vya wachimba madini. kuna baadhi ya miji huwa kama mji kwa ajili ya uchimbaji madini na wakazi wa maeneo hayo huwa ndio wanaochimba madini hayo kama ajira