Nyota nova : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 3:
 
==Historia ya utazamaji==
Zamani nyota zote zilizowaka hivi ziliitwa kwa jina lilelile "nova". Jina hili lilitumiwa mara ya kwanza na [[Tycho Brahe]] ambaye katika mwaka 1572 aliona nyota mpya katika eneo la kundinyota [[Mke wa Kurusi|Mke wa Kurusi ''(Cassiopeia)'']] na kueleza utafiti wake katika kitabu cha "De stella nova" <ref>Kilatini kwa "Kuhusu nyota mpya", linganisha [https://www.nasa.gov/mission_pages/WISE/multimedia/gallery/pia13119.html Tycho's Supernova Remnant], tovuti ya NASA, iliangaliwa Februari 2108</ref>. Wakati huo Tycho Brahe alianzisha majadiliano kuhusu mafundisho ya wataalamu wa kale walioamini kwamba hakuna mabadiliko yoyote kwenye anga ya nyota<ref>Majadiliani yaliendelezwa na [[Johannes Kepler]] aliyeandika mwaka 1606 pia kuhusu "Stella Nova in pede Sagitarii" (kuhusu nyota mpya mguuni pa kundinyota Kausi)</ref>.
 
Hata kabla ya Tycho kulikuwa na taarifa kuhusu nyota zilizotokea angani. Taarifa ya kale zaidi ni ya wanaastronomia nchini China kwenye mwaka 185 baada ya Kristo kuhusu "nyota geni" iliyoonekana karibu na [[Rijili Kantori|Rijili Kantori ''(α Centauri)'']]. Nova nyingine ilitazamiwa mwaka 1006 na kurekodiwa na wanaastronomia Wachina, Wajapani na Wakristo wa Baghdad. Mabaki yake huonekana hadi leo kama "Nebula ya Kaa" katika eneo la [[Tauri (kundinyota)|Tauri ''(Taurus)'']].