Nyota nova : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 9:
==Tofauti kati ya Nova na Supanova==
Tangu [[karne ya 20]] vipimo na elimu iliyopanuka vilifanya wanaastronomia kutofautisha kati ya "nova" na "supanova" ambazo zote ni "nyota mpya" zinazotokea angani kwa muda ila kwa sababu tofauti.
*Nova ya Tycho Brahe pamoja na ile ya mwaka 1006 siku hizi zinaitwa "[[supanova]]" maana zilikuwa ni milipuko ya nyota zilizoharibiwa wakati wa matukio haya. Inayobaki ni wingu la mata yake iliyosambaa katika eneo kubwa kama ile ya Nebula ya Kaa. Nishati inayopatikana katika mlipuko wa supanova inazidi ile ya kuwaka kwa nova mara nyingi, hivyo uteuzi wa jina la "supa"-nova (yaani nova kuu).
 
*Neno "nova" linafahamika sasa ni kuwaka kwa muda kwa nyota ndani ya [[nyota pacha|mfumo wa nyota pacha]]. Katika hali ya nova, nyota huongeza mwangaza ghafla mara elfu kadhaa ya kawaida yake hadi kurudi tena baada ya wiki au miezi katika hali yake kama kabla ya kuwaka. Pia hapa inawezekana kwamba wingu linabaki lakini nyota yenyewe bado iko.