Tofauti kati ya marekesbisho "Majadiliano ya mtumiaji:Unja1234"

no edit summary
Tag: 2017 source edit
::Asante kwa jibu. Wakati mwingine inaweza kutosha kutaja sababu kifupi tu kwenye muhtasari. Lakini mara nyingine na safari hii ingekuwa afadhali kusubiri majadiliano, hasa kama lemma imeshatumiwa mara nyingi. Pamoja na haya ukifanya utafiti lemma hii 1) haiko bado katika kamusi sanifu (niliyo nayo), 2) inapatikana kwa google search kwa maumbo yote mawili yaani Chansela na kansela, ingawa kwa sasa "kansela" ziko zaidi. Lakini kwenye maneno yasiyosanifishwa bado matumizi yanaweza kubadilika mwaka baada ya mwaka. Na hasa kama mifano ya google ni chache (kama hapa) hatuna takwimu ya kutegemea. Haya yote si msingi imara wa kubadilisha lemma. Katika wikipedia nyingine hapa kuna mara nyingi chanzo cha "edit war". Sisi tumefaulu kuepukana nayo kwa miaka yote kwa kuwasiliana kati yetu kwa heshima. Karibu kwenye ushirikiano! '''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 12:55, 28 Machi 2018 (UTC)
:::Nashukuru. Nilikuwa najua tu kuhusu neno 'kansela' pekee kwa vile hutumiwa katika DW.
::::Hi si ajabu. DW ni sauti ya Ujerumani. Maana Wa-TZ na Wa-EAK wanaotunga matini za DW-Kiswahili pale Cologne wamejifunza Kijerumani wakitumia neno "Kanzler" au "Kanzlerin" (kike). Hata "chansela" ni utohoaji tu wa neno la Kiingereza. Asili yake ni Kilatini "cancellarius" kwa lugha zote za Ulaya. Ila labda njia ya kupitia Kiingereza itaeleweka rahisi zaidi kwa wasomaji wetu Afrika ya Mshariki. Ni vema kutaja maumbo yote mawili na kutumia redirect. Ninanakili sehemu ya chini kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala tusikie kama wengine wana neno kama ibaki Kansela caadaye kazi kwako kubadilisha makala zote) au irudishwe Chansela.'''[[Mtumiaji:Kipala|Kipala]] ([[Majadiliano ya mtumiaji:Kipala|majadiliano]])''' 19:29, 28 Machi 2018 (UTC)