Utume wa Yesu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 19:
 
Utume wake wa mwisho mjini Yerusalemu ulianza na tukio la [[Jumapili ya matawi|kuingia Yerusalemu kwa shangwe]] ya [[Wayahudi]] walioamini kwamba ndiye [[Masiya]], hasa baada ya [[muujiza]] mkuu alioufanya, yaani kumfufua [[Lazaro wa Bethania]] kutoka [[kaburi]]ni siku ya [[nne]] baada ya [[kifo]]. Injili zinasimulia kirefu zaidi habari za hiyo [[Juma Kuu|wiki ya mwisho]] kutokana na umuhimu wake kama kilele cha yote.<ref name=Turner613 >''Matthew'' by David L. Turner 2008 ISBN 0-8010-2684-9 page 613</ref>
 
==Ushahidi wa Petro==
Mtume Petro alisimulia kifupi utume wa Yesu kama ifuatavyo ([[Mdo]] 10:34-43):
 
34 Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; 35 bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye. 36 Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli akihubiri habari njema ya amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote), 37 jambo lile ninyi mmelijua, lililoenea katika Uyahudi wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo aliouhubiri Yohana; 38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye. 39 Nasi tu mashahidi wa mambo yote aliyoyatenda katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini. 40 Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu, akamjalia kudhihirika, 41 si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndio sisi, tuliokula na kunywa pamoja naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu. 42 Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa walio hai na wafu. 43 Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.
 
==Picha==