Malaika : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Ángel de la Independencia (cropped).jpg|thumb|malaikaMalaika wa [[uhuru]].]]
'''Malaika''' katika [[imani]] ya [[dini]] mbalimbali, kama vile [[Uyahudi]], [[Ukristo]] na [[Uislamu]] ni [[kiumbe]] wa kiroho tu anayeweza kutumwa na [[Mungu]] kwa [[binadamu]].
 
Kwa [[umbile]] lake hawezi kujulikana kwa [[hisi]] za [[mwili]] wetu.
 
Katika [[Biblia]] watatu tu wanatajwa kwa jina: [[malaika Mikaeli]], [[malaika Gabrieli]] na [[malaika Rafaeli]] (huyo katika [[Deuterokanoni]] tu).
 
Katika Uislamu ni kiumbe chepesi ambacho kimeumbwa kwa [[moto]] nacho huwa hakanyagi chini kama mwanadamu, bali huelea juu au kuketi ndani ya [[moyo]] wa mwanadamu.
 
==Katika Biblia==
Katika Biblia, malaika na watu ndio viumbe pekee vyenye [[hiari]] ya kuchagua wenyewe wachangie mpango wa Mungu au la. “Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi, chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako” ([[Kumb]] 30:19-20).
 
Malaika na watu wanaweza kuchagua hata wawe wema au wabaya [[milele]]. “Kulikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni” ([[Ufu]] 12:7-8). Chaguo letu binadamu linafanyika [[siku]] kwa siku kwa kuchukua misimamo mizuri au mipotovu kuhusu [[dini]] na [[maadili]]. “Mwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima” ([[Yoh]] 5:39-40).
 
Kati ya viumbe mbalimbali Mungu ameweka mpango: alitaka malaika wasioonekana wamtumikie kwa kutusaidia sisi watu, na vile vinavyoonekana tuvitumie kwa [[uadilifu]] ili kwa njia yetu vimtukuze yeye. “Atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote” ([[Zab]] 91:11). “Kwa Hekima yako ulimwumba mwanadamu, ili avitawale viumbe vilivyoumbwa nawe, na kumiliki ulimwengu katika utakatifu na kwa haki” ([[Hek]] 9:2-3).
 
Malaika ni [[roho]] tupu walioumbwa na Mungu ili wamtukuze milele, wamlinde kila mtu na kumtumikia [[Bwana]] [[Yesu]] katika kutuokoa. “Angalieni, msidharau mmojawapo wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni” ([[Math]] 18:10).
 
{{mbegu-dini}}
 
[[Jamii:Dini]]