Ufunuo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 3:
Ni kwamba katika [[dini]] mbalimbali kuna [[imani]] ya kwamba Mungu anaweza kujifunua kwa binadamu na kuwafunulia matakwa yake kwao.
Pengine ufunuo huo unakuja kuandikwa katika [[kitabu]] kitakatifu, kama vile [[Biblia]] kwa [[Wayahudi]] na [[Ukristo|Wakristo]], na [[Torati]], [[Zaburi]], [[Injili]] na [[Kurani]] kwa [[Uislamu|Waislamu]].
 
Ufunuo una umuhimu mdogo katika dini nyingine, isipokuwa katika [[Ubuddha]].
Mstari 35:
== Ukristo ==
Wakristo wanapokea ufunuo wa Mungu kwa taifa la [[Israeli]], wakiona ujio wa [[Yesu]] kuwa ndio [[kilele]] chake, ambapo Mungu alijifunua si kwa njia ya manabii, bali kwa njia ya [[Mwana]] wake, aliye [[Neno wa milele]]. Katika yeye ufunuo umekamilika usiweze kuboreshwa tena. Ufunuo huo unajitokeza hasa katika [[Agano Jipya]].
 
Kwa [[imani]] hiyo, Mungu aliwahi kujifunua kwa [[wazazi]] wetu wa kwanza, [[Adamu]] na [[Eva]], akaendelea hasa kwa [[taifa]] la [[Israeli]], hadi alipomtuma [[Mungu Mwana|Mwanae]] ajifanye mtu wa taifa hilo teule. “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana” ([[Eb]] 1:1-2).
 
Baada ya hapo, ufunuo wa Mungu hauendelei, kwa sababu alikwisha kuukamilisha kwa kumtuma duniani [[Neno la Mungu|Neno]] wake wa [[milele]]. “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua” ([[Yoh]] 1:17-18). Baada yake hauwezekani ufunuo mpya. Hatutakiwi kumuamini yeyote akidai eti, ametumwa kukamilisha kazi ya Yesu; kwa kuwa mwenyewe alisema, “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe” ([[Math]] 24:35). “Ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe! Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe!” ([[Gal]] 1:8-9).
 
Ufunuo huo wa Mungu unatufikia kupitia [[Kanisa]] lake, lililokabidhiwa [[Mapokeo ya Mitume]] na linaloongozwa na [[Roho Mtakatifu]] hadi [[ukweli]] wote. Yesu aliahidi kwamba, “Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake” (Yoh 16:13). “Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu” ([[1Kor]] 2:10).
 
Katika [[teolojia]] ya [[Ukristo|Kikristo]] [[neno]] ufunuo lina maana ya jumla ya [[dogma]] zote, yaani kweli zilizofunuliwa na zinazodai imani ya kila mtu ili kupata [[wokovu]].
Line 40 ⟶ 46:
Kwa [[Kanisa Katoliki]] kweli hizo zinapatikana katika [[Biblia]] pamoja na [[Mapokeo]] ya [[Mitume wa Yesu|Mitume]] vinavyofafanuliwa na [[Ualimu wa kanisa]].
 
Kanisa Katoliki linatofautisha pia huo [[ufunuo wa hadhara]] na [[mafunuo ya binafsi]] ambaoambayo si lazima watu wengine wayasadiki.
 
== Uislamu ==
[[Uislamu]] pia unakubali ufunuo wa Mungu kwa Wayahudi kupitia manabii, Isa (Yesu) akiwa mmojawao, lakini unaamini ufunuo huo umekamilishwa kupitia [[Muhammad]], nabii wa mwisho na mkuu kuliko wote, na umeandikwa katika [[Kurani]], inayohesabiwa "neno la Mungu" kwa maana kamili, kwa kuwa limetoka kwake na kuandikwa bila mabadiliko.
 
{{mbegu-dini}}
 
[[Jamii:Dini]]