Ufunuo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 40:
Baada ya hapo, ufunuo wa Mungu hauendelei, kwa sababu alikwisha kuukamilisha kwa kumtuma duniani [[Neno la Mungu|Neno]] wake wa [[milele]]. “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua” ([[Yoh]] 1:17-18). Baada yake hauwezekani ufunuo mpya. Hatutakiwi kumuamini yeyote akidai eti, ametumwa kukamilisha kazi ya Yesu; kwa kuwa mwenyewe alisema, “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe” ([[Math]] 24:35). “Ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe! Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe!” ([[Gal]] 1:8-9).
 
===Msimamo wa Kanisa Katoliki===
Ufunuo huo wa Mungu unatufikia kupitia [[Kanisa]] lake, lililokabidhiwa [[Mapokeo ya Mitume]] na linaloongozwa na [[Roho Mtakatifu]] hadi [[ukweli]] wote. Yesu aliahidi kwamba, “Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake” (Yoh 16:13). “Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu” ([[1Kor]] 2:10).
 
Hivyo tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila kudanganyika. Yesu aliwaambia [[Mitume wa Yesu|Mitume wake]], “Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma” ([[Lk]] 10:16). “Sisi nasi twamsukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kwelikweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini” ([[1Thes]] 2:13).
 
Tukipata mafundisho ya Kanisa tunapaswa kuyasadiki kwa moyo mmoja tupate uzima wa milele, kwa kuwa Yesu aliwaambia Mitume, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa” ([[Mk]] 16:16).
 
Tunapaswa kusadiki hasa [[Utatu]] wa Mungu pekee, kwamba ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. [[Milele]] yote Baba kwa jinsi alivyo ndani mwake anamzaa Mwana na kumvuvia [[Roho Mtakatifu]], kama vile [[jua]] linavyotoa [[mwanga]] na [[joto]] lisitenganike navyo. Mwana, ambaye “ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake” ([[Eb]] 1:3), alisema: “Nimekuja kutupa moto duniani” (Lk 12:49). Naye Roho aliwashukia wafuasi wake “kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu” ([[Mdo]] 2:3-4).
 
Katika [[teolojia]] ya [[Ukristo|Kikristo]] [[neno]] ufunuo lina maana ya jumla ya [[dogma]] zote, yaani kweli zilizofunuliwa na zinazodai imani ya kila mtu ili kupata [[wokovu]].