Utatu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 16:
==Katika matamko rasmi ya Kanisa==
Imani hiyo ilizidi kufafanuliwa hasa katika [[karne IV]], [[mitaguso]] [[Mtaguso Mkuu|mikuu]] ya kwanza ilipochukua msimamo dhidi ya [[wazushi]] waliokanusha [[umungu]] wa Yesu na wa Roho Mtakatifu. Ilipata muundo wa kudumu katika [[Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli]] inayotumika hadi leo katika [[madhehebu]] mengi ya [[Ukristo]].
 
Kwa imani hiyo tunapaswa kusadiki hasa Utatu wa Mungu pekee, kwamba ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Milele yote Baba kwa jinsi alivyo ndani mwake anamzaa Mwana na kumvuvia Roho Mtakatifu, kama vile jua linavyotoa mwanga na joto lisitenganike navyo. Mwana, ambaye “ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake” ([[Eb]] 1:3), alisema: “Nimekuja kutupa moto duniani” ([[Lk]] 12:49). Naye Roho aliwashukia wafuasi wake “kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu” ([[Mdo]] 2:3-4).
 
Mungu hagawanyiki hata kidogo, bali daima ni [[Umoja]] kamili. “Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja” ([[Mk]] 12:29). [[Ibada|Tumuabudu]] yeye peke yake katika nafsi tatu, na Utatu wa nafsi katika Umoja wa hali yake, tusichanganye nafsi wala kugawa Umungu. Baba si Mwana wala Roho Mtakatifu. Mwana si Baba wala Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu si Baba wala Mwana. Lakini milele yote nafsi hizo tatu ni Mungu yuleyule pasipo tofauti ya kuzitenganisha: kila moja imo ndani ya nyingine. “Mimi na Baba tu umoja” ([[Yoh]] 10:30).
 
Tumejua kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu kwa sababu Baba aliwatuma kwetu Mwanae na Roho Mtakatifu. “Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake. Na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, ‘Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye’” ([[Math]] 3:16-17). Naye akaagiza, “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu” (Math 28:19). Ni nafsi tatu zenye [[jina]] moja, yaani Umungu mmoja tu.
 
Umoja wa Mungu unategemea hasa kwamba Mwana na Roho Mtakatifu wanachanga Umungu wa Baba, ambaye wanatokana naye pasipo utengano wowote. Baba anajifahamu na kujipenda: wazo analojifahamu ndiye Mwana, upendo anaojipenda katika wazo hilo ndiye Roho Mtakatifu. “Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu” (Yoh 17:24).
 
Nafsi tatu za Mungu zina Umoja hata katika utendaji, kila nafsi akiuchangia kulingana na sifa yake maalumu ndani ya Utatu. Baba Mwenyezi sifa yake ni [[Uwezo]]. Mwana kama Neno la Baba sifa yake ni [[Hekima]]. Roho kama [[Pumzi]] ya [[uhai]] ya Baba sifa yake ni [[Upendo]]. Katika Uwezo wake Baba anafanya yote kwa Hekima na Upendo, hasa katika [[Utume wa Yesu|utume wa Mwana]] aliyefanyika mtu na katika utume wa Roho kama paji. “Amin, amin, nawaambia: Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vilevile” (Yoh 5:19).
 
==Katika liturujia==