Mauti : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 28:
# Kifo ni kupita penginepo: [[uzima wa milele]], [[mbinguni]], upeo wa wafu n.k.
 
==Katika Ukristo==
{{mbegu-biolojia}}
Hasa kadiri ya [[Ukristo]], ni muhimu tujiandae kufa wakati wowote na namna yoyote kwa kuishi kitakatifu sasa na kwa kujiombea [[neema]] tutakazohitaji saa ya kufa kwetu, tukijua tumewekewa “kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu” ([[Eb]] 9:27). “Katika mambo yako yote uukumbuke mwisho wako, hivyo hutakosa kamwe hata hatima” ([[YbS]] 7:36). “Hamjui yatakayokuwako kesho! Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka” ([[Yak]] 4:14). “Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni” ([[Math]] 26:41).
 
“Ina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wake” ([[Zab]] 116:15). Hasa [[utiifu]] wa [[Yesu]] [[Msalaba|msalabani]] umegeuza [[laana]] ya kifo iwe [[baraka]] kwa waamini wake. “Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao” ([[Ufu]] 14:13).
 
Tutakapofariki [[dunia]] [[roho]] yetu isiyokufa, mbali na [[mwili]] unaooza, itapewa [[tuzo]] au [[adhabu]] tuliyostahili kwa [[maisha]] yetu. “Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake” ([[Lk]] 16:22-23). “Kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida… ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo, maana ni vizuri zaidi sana” ([[Fil]] 1:21,23). “Nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana” ([[2Kor]] 5:8). Kwa kuwa kifo ni “mavumbi kuirudia nchi kama yalivyokuwa, nayo roho kumrudia Mungu aliyeitoa” ([[Mhu]] 12:7). [[Kiyama|Siku ya ufufuo]] roho na mwili vitaungana tena kwa ajili ya [[uzima]] au [[moto]] wa [[milele]]. “Pumzi iliwaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno” ([[Ez]] 37:10).
 
{{mbegu-biolojia}}
 
[[Jamii:Biolojia]]