'''Sokrates''' ({{lang-grc|Σωκράτης|Sōkrátēs}}, 470–399[[470 KK]] – [[399 KK]]) alikuwa [[mwanafalsafa]] [[Ugiriki|Mgiriki]] ([[mtu]] wa [[Athens]]), [[falsafa|mwanafalsafa]]. <ref>[[Anthony Gottlieb]] alimwita shahidi na mtakatifu wa falsafa (Monk & Raphael, 2000)</ref>
Nje ya [[falsafa]], anajulikana hasa kwa [[kifo]] chake. Alifariki kutokana na kunywa [[sumu]] baada iliyokuwa [[adhabu]] yake kwa kupatikana na hatia katika [[mahakama]] ya watu wa Athens. Ilidaiwa kwamba mafunzo yake yaliingilia [[dini]] ya mji wa Athens na kulipotoshakupotosha [[vijana]] wake. Ingawa alipewa nafasi kutoroka ili kuepukana na [[hukumu]] yake na kwenda [[uhamisho|uhamishoni]], Sokrates alichagua kunywa sumu hiyo kwa sababu alikuwa amekubali kwa [[hiari]] yake afuate [[sheria]] za Athens, na akaamini kwamba angalikwepa hukumu yake angaliuaibisha [[mkataba]] huo.
Maarifa mengi kuhusu Sokrates yametokea mazungumzokatika [[majadiliano]] yaliyoandikwa na [[Plato]], [[mwanafunzi]] wake na mwanafalsafa, maandiko ya [[Zenephon]], mtu wa [[rika]] lake, [[Aristofanes]], na [[Aristotle]]. Kuna matatizo katika maandiko yanayomhusu Sokrates, hivyo siosi vyema kutegemea chanzo kimoja tu. Ukitazama mambo yanayofanana baina ya maandiko, na ukaachilia mbali mambo yanayofikiriwa kuongezwa na [[mwandishi]], Sokrates mwenyewe ataonekana.