Aristoteli : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 29:
Aristoteli alikusanya [[elimu]] ya wakati wake akajaribu kuipanga katika utaratibu.
 
Mwenyewe alifundishwa na Plato lakini alitofautiana na mwalimu wake katika mafundisho juu ya tabia za vitu vyenyewe. Plato aliona ya kwamba ujuzi wote tunaopata kupitia [[hisi|milango yetu ya utambuzifahamu]] hukosa uhakika, si kamili; ujuzi wa kweli unapatikana kwa njia ya roho inayoweza kuelewa kiini cha kitu, wakati milango ya utambuzi inaona [[umbo]] la nje tu. Aristoteli alifikiri tofauti akaona utambuzi kupitia milango yetu ni muhimu zaidi na ujuzi hutegemea utazamaji wa mazingira.
 
Katika "metafizikia" yake kuna pia dhana juu ya "mwanzilishi" au "mwenye mwendo wa kwanza". Aliona kwamba kila kitu kina mwendo kilichosababishwa na kitu kingine. Hivyo [[mantiki]] yake ilidai kuwepo kwa chanzo cha mwendo wote akakiita "mwendeshaji asiyeendeshwa" (kwa [[Kigiriki]] ''proton kinoun akineton'') au kwa lugha nyingine "chanzo asilia". Chanzo asili hiki kwake ni roho au dhana yenyewe (kwa Kigiriki ''nous''). Aristoteli aliweza kukiita pia "Mungu".