Tofauti kati ya marekesbisho "Demokrasia"

140 bytes added ,  miaka 4 iliyopita
No edit summary
 
== Aina za Demokrasia ==
# ''Demokrasia ya moja kwa moja'' (kwa [[Kiingereza]] "Direct Democracy") ni aina ya demokrasia ambayo wananchi wote wanaweza kushiriki katika kuamua masuala ya kisiasa, ya kijamii, ya kisheria na ya kiuchumi bila kutumia chombo cha uwakilishi kama vile [[bunge]]. Uwezo huu wa wananchi kutoa maamuzi unaweza kuwapa hata uwezo wa [[Mahakama|kimahakama]], ingawa mara nyingi wananchi hupewa uwezo wa kutunga au kupitisha sheria tu. Demokrasia ya moja kwa moja ni tofauti na demokrasia inayofuatwa katika nchi nyingi [[duniani]] hivi sasa, ambapo wananchi huchagua wawakilishi wao katika [[uchaguzi]]. Nchi ya Uswisi ni maarufu kwa mfumo wake wa demokrasia ya moja kwa moja ambako sheria nyingi zinaamuliwa na wananchi wote kwa njia ya kura.
# ''Demokrasia shirikishi'' ("Representative Democracy"): hapo wachache hupewa na wengi [[dhamana]] katika uwakilishi wa jamii katika maamuzi. Wachache huchaguliwa na wengi kwa njia ya demokrasia huru na ya [[haki]] kwa kufuata [[Katiba]] ya nchi hiyo. Mfano: Wabunge huwakilisha wananchi wao katika kuleta [[maendeleo]] na kuishauri serikali juu ya maendeleo ya nchi yao.