Saa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 5:
Saa inagawiwa kwa [[dakika]] 60 na [[sekundi]] 3,600. [[Siku]] ina takriban masaa 24.
 
Asili ya hesabu ni katika utamaduni wa [[Sumeri]] na [[Misri ya Kale]] uliogawa mchana na pia usiku kwa vipindi vya masaa 12.
 
== Historia ==
 
=== Saaa ya mkono ===
Dhana ya saa ya mkono ina historia ndefu toka wakati wa uzalishaji wa saa za mwanzo kabisa katika karne ya 16. [[Malkia Elizabeth I]] wa [[Uingereza]] alipokea saa ya mkono kutoka kwa [[Robert Dudley]] mnamo mwaka wa 1571. Saa ya mkono ya zamani kabisa iliyopo hadi hivi sasa (iliyokuwa ikiitwa saa ya bangili) ilitengenezwa mwaka 1806. Mwanzoni saa za mkono zilikuwa zikivaliwa na wanawake tu, wakati wanaume walikuwa wakitumia saa za mfukoni hadi karne ya 20.<ref name="Evolu">{{cite web|url=http://www.vintagewatchstraps.com/wristwatches.html|title=The Evolution of the Wristwatch}}</ref>
[[File:Campaign Watch 1915.jpg|thumb|right|Tangazo la saa inayotengenezwa na[[Mappin & Webb]] mwaka 1898.]]
 
Saa za mkono zilianza kuvaliwa na wanaume wanajeshi mwisho mwa karne ya 19 kwa ajili ya kupanga vyema vita. Kampuni ya Garstin ya London ilipata hati miliki ya "Watch Wristlet" mwaka 1893, lakini walikuwa wakitengeneza saa miundo kama hiyo tangu miaka ya 1880. Maofisa wa Jeshi la Uingereza walianza kutumia saa za mkonononi wakati wa kampeni ya kijeshi ya kikoloni katika miaka ya 1880, kama vile wakati wa [[Vita ya Anglo-Burma]] ya 1885.<ref name="Evolu" /> Wakati wa [[Vita ya kwanza ya Makaburu]], umuhimu wa kuratibu harakati za vikosi na kusawazisha mashambulizi dhidi ya [[Makaburu]] ulikuwa muhimu sana, na matumizi ya saa za mkono ulianza kuenea miongoni mwa maofisa wa kijeshi. Kampuni ya [[Mappin & Webb]] ilianza uzalishaji wa saa za wanajesho wakati huko Sudan mnamo mwaka 1898 na kuongeza kasi ya uzalishaji wakati wa [[Vita ya Pili ya Makaburu]] miaka michache baadaye. Katika bara la Ulaya kampuni ya [[Girard-Perregaux]] na kampuni nyingine za Uswisi zilianza kutengeneza saa za mkono za maofisa wa jeshi la Ujerumani mwaka 1880.
 
Kawaida saa ubora wa saa unahusishwa na mambo mbalimbali kama vile saa inavyoweza kuzuia maji. Shirika la Kimataifa la Usanifishaji (kwa kifupi ISO) limetoa vipimo maalum vya saa zinavyozuia maji.
 
 
==Marejeo==
{{Marejeo}}
 
== Viuongo vya nje ==
 
* [http://www.watkinsr.id.au/david.html Utengenezaji saa za Kimarekani na Kiswisi mwaka 1876]
* [http://www.sil.si.edu/digitalcollections/HistoryCultureCollections/SIL-029-015/pdf/SIL-029-015.pdf Kampuni za zamana na sasa za kutengeneza saa Marekani]
* [http://www.fhs.ch/ Shirikisho la Kampuni za Saa Uswisi]
* [https://greatwatches.nyc/atm-water-resistance/ Vipimo vya saa kuzuia maji]
* [https://www.nytimes.com/2013/10/23/fashion/wrist-watches-from-battlefield-to-fashion-accessory.html Historia ya saa toka kwenye uwanja wa vita hadi kwenye mitindo]
* [http://www.historyofwatch.com/ Historia ya saa ya mkono na saa ya ukutani]
 
 
 
{{mbegu-sayansi}}