Madhehebu : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 1:
[[File:Prevailing world religions map.png|thumb|400px|Dini na madhehebu yake leo ulimwenguni]]
'''Madhehebu''' (kutoka [[Kar.Kiarabu]] مذهب ''madhhab'') ni mafundisho, [[maadili]] na matendo ya [[ibada]] yaliyo ya msingi katika [[dini]] fulani.
 
Hutumiwa pia kutaja [[Kundi|makundi]] ndani ya [[dini]] fulani ambayo yanatofautiana bila ya kuvunja [[umoja]] wa msingi.
 
[[Historia]] inashuhudia hata leo kwamba madhehebu mbalimbali ya dini ileile yanaweza kushindana hata kupigana [[vita]].
 
==Asili ya neno==
Kiasili neno la Kiarabu ''madhhab'' limetaja makundi ndani ya mafundisho ya masharti ya [[Uislamu]] yaliyotofautiana juu ya vipengele fulani vya [[shari'a]]. Likaendelea kutumiwa kutaja pia makundi makubwa ndani ya [[Ukristo]] na baadaye katika [[dini]] nyingine.
 
Kiasili neno la Kiarabu ''madhhab'' limetaja makundi ndani ya mafundisho ya masharti ya Uislamu yaliyotofautiana juu ya vipengele fulani vya [[shari'a]]. Likaendelea kutumiwa kutaja pia makundi makubwa ndani ya Ukristo na baadaye katika dini nyingine.
 
==Madhehebu katika Ubanyani==
Katika [[Ubanyani]], tofauti ya madhehebu inategemea [[mungu]] yupi anaheshimiwa zaidi kati ya [[miungu]] mingi inayosadikiwa na waumini wa dini hiyo. Ndivyo yanavyotajwa [[Shaivism]], [[Shaktism]], [[Vaishnavism]], [[Smartism]] na [[Halumatha]].
 
==Madhehebu katika Uyahudi==
Wakati alipoishi [[Yesu Kristo]], dini ya [[Uyahudi]] ilikuwa na madhehebu yaliyoshindana sana, hasa [[Masadukayo]], [[Mafarisayo]] na [[Waeseni]].
 
Baada ya [[mwaka]] [[70]], [[Yerusalemu]] na [[hekalu]] lake vilipobomolewa, walibaki Mafarisayo tu, lakini leo Wayahudi wanatofautiana tena hasa kati ya walioshikilia [[imani]] sahihi]] kadiri ya [[mapokeo]] na wale wanaotaka kujilinganisha zaidi na hali ya [[ulimwengu]] wa kisasa.
 
==Madhehebu katika Ukristo==
Wafuasi wa dini ya [[Ukristo]], kutokana na [[wingi]] wao katika [[urefu]] wa [[historia]] na [[upana]] wa [[jiografia]], wamegawanyika katika madhehebu mengi, kuanzia [[Kanisa Katoliki]], [[Waorthodoksi]] na [[Waorthodoksi wa Mashariki]] hadi makundi maelfu[[elfu]] kadhaa ya [[Uprotestanti]] ambayo yalitokea hasa kuanzia [[karne XVI]] na yanazidi kuongezeka siku kwa siku.
 
Pengine madhehebu kadhaa yanayojitegemea yanaweza kutazamwa kama jamii moja kutokana na asili, historia na misimamo yake (k.mf. Ushirika wa [[Anglikana]] au [[Makanisa Katoliki ya Mashariki|riti za mashariki]] na [[Kanisa la Kilatini|magharibi]] za Kanisa Katoliki).
 
Baadhi ya Wakristo wanaona ma[[farakano]] hayo kuwa mabaya sana, wakizingatia ombi la [[Yesu]] kwamba wafuasi wake wawe na [[umoja]] ili [[ulimwengu]] upate kumuamini. Kwa sababu hiyo wanashughulikia [[ekumeni]] ili kurudisha umoja kamili kati yao bila kufuta tofauti zisizovuruga umoja wa msingi.
 
==Madhehebu katika Uislamu==
Line 31 ⟶ 30:
 
Kati ya Wasunni kuna madhehebu au madhhab manne yanayokubaliwa rasmi. Hali halisi makundi mengine ya Kisunni kama [[Wahabiyya]] yanaweza kuitwa madhehebu pia. Madhehebu manne yanayokubaliwa kati ya Wasunni ni [[Washafii]], [[Wahanbali]], [[Wamaliki]] na [[Wahanefi]] yaliyopokea majina kutokana na walimu wakuu wa kihistoria [[Muhammad ibn ldris ash-Shafi'i]], [[Ahmad ibn Hanbal]], [[Malik ibn Anas]] na [[Abu Hanifa]].
{{mbegu-dini}}
 
[[Jamii:Dini]]
[[Jamii:Uhindu]]