Mifugo : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa umeelekezwa kwenda Wanyama wa nyumbani
Removed redirect to Wanyama wa nyumbani
Tag: Removed redirect
Mstari 1:
'''Mifugo''' au '''Wanyama wa kufugwa''' ni [[wanyama]] wanaopatikana kutokana na ufugaji wa kibinadamu.
#REDIRECT[[Wanyama wa nyumbani]]
 
Wako tofauti na [[wanyama wa pori]] baada ya na mchakato mrefu ambako wanyama wa pori ama walijiunga na binadamu au walishikwa nao na watoto wao kuteuliwa kutokana na tabia zilizopendelewa na wafugaji wao. Tabia hizi ni pamoja na upole na uwezo wa kupatana na binadamu, uwezo wa kuzalisha kiasi fulani cha nyama au maziwa, uwezo wa kustawi kwa chakula fulani au katika mazingira mbalimbali.
Katika mchakato wa vizazi vingi tabia zilizolengwa ziliimarishwa katika spishi zinazofugwa.
 
Uteuzi huu umesababisha tofauti za kimaumbile na tofauti za tabia baina ya wanyama wa kufugwa na wanyama wa pori wa spishi ileile. Tofauti hizi zinaonekana katika rangi, ukubwa wa mwili, uwezo wa kuwasiliana na binadamu na mengine.
 
 
Imethibtishwa ya kwamba mnyama wa kwanza wa kufugwa alikuwa mbwa. Asili ya mbwa walikuwa vikundi vya mbwa mwitu wa Ulaya (wolf) waliofuata koo za binadamu wawindaji na kula mabaki ya chakula yaliyotupwa nao. Kwa kupatana na mbwa mwitu ambao walikuwa wapole na kutoshambulia watu (na kuua wote waliokuwa wakali) binadamu hao walianza kupatana nao na kuona faida ya uangalivu wao wakati mgeni au windo alikaribia. Tangu kuwapatia mbwa mwitu chakula kama zawadi waliendelea kuzoeana. Ingawa historia hii bado haieleweki kikamilifu watalaamu wengine wanaona ya kwamba wawindaji kadhaa walianza kutunza watoto wa mwbwa mwitu kwao na kuwafuga kama wanyama wapenzi.
 
Inaonekana ya kwamba kulikuwa pia na wanyama wengine wa porini waliofuata binadamu kwa sababu waliona faida kukaa karibu nao kama vile paka (aliyefuata panya waliokula mavuno ya wakulima wa kwanza).
 
Vilevile asili ya kuku ni kuku mwekundu wa porini wa Indonesia (red junglefowl) aliyetafuta takataka kwenye makazi ya watu, akawazoea na kutumiwa nao kama chanzo cha nyama na mayai.