Tamthilia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 25:
 
{{mbegu-fasihi}}
'''Mabadiliko na maendeleo ya tamthiliya'''
[[Jamii:Fasihi]]
 
Kwa kutumia muundo wa Shakespeare, waandishi waliandika tamthiliya kwa lugha ya Kiswahili na zilihusisha maswala ya Kiafrika. Wakati wa wakoloni, drama ilikuwa kwa ajili ya Wazungu na Waafrika wachache waliojua Kizungu. Baadaye, waandishi wazalendo waliotaka kuwasiliana na umma, iliwabidi watunge tamthiliya yao kwa lugha ya Kiswahili. Baadaye, liche ya tamthiliya kuzingatia matumizi ya lugha ya Kiswahili, walianza kuzitazama, kuchunguza na kuzifanyia majaribio.
 
Tamthiliya za awali k.v. Wakati Ukuta na Heshima Yangu hazikuwa na utohozi wa matumizi ya fani za sanaa za maonyesho ya jadi. Kuanzia mwishoni mwa miaka 60, na mwanzoni mwa miaka 70, tamthiliya zilianza kuonyesha mwelekeo mpya. Pia, falsafa na imani za Kiafrika kabla ya ubepari zilianza kudidimia kidogo.
 
'''Historia ya tamthiliya kwa mujibu wa Syango na Mazrui (1992)'''
 
Hawa walipanga kazi ya historia ya tamthiliya katika makundi manne:
 
# '''Tamthiliya za kwanza kuchapishwa zilikuwa kati ya miaka 50-60'''
 
Baadhi ya tamthiliya hizo ni kama- Nakupenda Lakini... (Henry Kuria, 1957), Afadhali Mchawi, na pia Mgeni Karibu (Graham Hyslop, 1957), Nimelogwa Nisiwe na Mpenzi (Ngugi 1961). Zilizungumzia maswala ya jamii chache zikiwa za upelelezi. Tamthilya zingine zilizungumzia maswala ya kutovunja sheria zikirejelea wageni wakoloni. Pia zilibainisha mgongano baina ya jamii za makabila tofauti tofauti. nyingi zilikuwa na lengo za burudani. Na pia ziliendelea kudunisha hadhi ya Waafrika hata ingawa ni za Kiswahili. Mwaka 1960 ndipo Little Theatres zilianzishwa kwa burudani kwa Wazungu.
 
2. '''Tamthiliya baada ya miaka 60'''
 
Tamthiliya hizi zilijaa maudhui ya kimapenzi, migogoro ya kitamaduni, maudhui ya kikoloni. Tamthiliya hizi ni kama vile Wakati Ukuta na Kwenye Ukingo wa Thim (Hussein Ibrahim), Pambo (Peninah Muhando), na Tazama Mbele (Kitsau Jay).
 
3. T'''amthiliya za Mwisho wa 60 na mwanzo wa 70'''
 
Maudhui yalikuwa: maswala ya ukoloni, historia ya Waafrika katika mapinduzi, haki za wanyonge. Kwa mfano, Mzalendo Kimathi (Ngugi), Mkwawa wa Hehe.
 
4. '''Tamthiliya za 70 hadi sasa'''
 
Zilikuwa na mwamko mpya. Zilichunguza jamii za Afrika Mashariki kwa mkondo mpya. Zilizungumzia: ukoloni mamboleo, uongozi, siasa na matatizo mengine kama vile ufisadi, unyanyasaji, uporaji n.k. Kwa mfano; Aliyeonja Pepo (Faruk Topan), Mashetani (Ibrahim Hussein), Kilio cha Haki (Alamin Mazrui).
[[Jamii:Fasihi]]
[[Jamii:Tamthilia|*]]