Tofauti kati ya marekesbisho "Carolyne Ekyarisiima"

1,200 bytes added ,  miaka 3 iliyopita
no edit summary
'''Carolyne Ekyarisiima''' (amezaliwa tar. 20,juni,1986) ni mjasiriamali,mwanasayansi katika nyanja ya kompyuta na mwasisi wa [[shirika]] lisilokuwa la kiserikali la '''''apps and girls''''' lenye malengo ya kuongeza idadi ya wanawake kutumia Teknohoma kutengeneza miradi ya kusaidia jamii zao<ref> https://www.dailynews.co.tz/news/uwekezaji-katika-teknolojia-ya-mawasiliano-kwa-wanawake-ni-muhimu.aspx </ref> .
Kupitia taasisi yake ya ''apps and girls'' anatoa semina na mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi waliopo katika shule za sekondari, pia ameanzisha klabu za kujifunza mambo ya teknolojia katika mashule ,ambapo kupitia klabu hizi wanafunzi hukutana kujifunza na kushirikishana mambo mbalimbali yahusuyo teknohama.
Wasichana wameweza kujifunza namna ya kutengeneza tovuti ,programu za kwenye simu janja na pia wanajifunza namna ya kuweza kujieleza mbele ya wafadhili wanapokuwa wanataka kuomba pesa kwa ajili ya kuendeleza programu zao .<ref> https://qz.com/africa/1214051/how-tanzania-is-betting-on-coding-to-help-close-the-gender-gap-in-its-tech-sector/ </ref>
 
==Maisha yake==
Alizaliwa wilayani [[Bushenyi]] nchini [[Uganda]] katika [[familia]] ya watoto saba yeye akiwa mtoto wa tano.
Alitumia mda wake mwingi kuchunga [[ng’ombe]],lakini pia aliweza kupata mda wa kwenda shule kwa kuwa baba yake alikuwa ni Mwalimu wa Shule ya msingi na alithamini sana elimu.<ref>https://www.africanindy.com/business/the-digital-changemaker-1627779</ref>
 
==Elimu yake==
'''Carolyne''' ana shahada ya sayansi ya kompyuta na shahada ya uzamili ya mifumo ya habari(information systems) kutoka katika chuo cha kimataifa cha Kampala.<ref>https://www.irex.org/people/carolyne-ekyarisiima</ref>
 
==Tuzo Mbalimbali==
aliwahi kujishindia pesa kiasi cha dola 25000,zilizokuwa zikitolewa na [[Tigo]] kwa ajili ya kudhamini watu wanao jihusisha na kuleta mabadiliko ndani ya jamii kupatia [[teknolojia]].<ref>https://www.dailynews.co.tz/news/uwekezaji-katika-teknolojia-ya-mawasiliano-kwa-wanawake-ni-muhimu.aspx</ref>
aliweza kutajwa kama mmoja wa wavumbuzi bora 20 wa mwaka,waliokuwa wakiwania tuzo hiyo(innovator of the year award)inayo tolewa na '''AIDF''' <ref>http://africa.aidforum.org/news/innovator-of-the-year-award-finalists-announced</ref>
 
 
 
==Elimu yake==
{| style="font-size:90%; width: 65%; padding: 3px; margin: 0 auto;" class=toccolours
|-