Waha : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Masahihisho aliyefanya Mtongori (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Riccardo Riccioni
No edit summary
Mstari 22:
 
[[Utamaduni]] wao, yaani ma[[vazi]] yao ilikuwa ni magome ya [[miti]] yaliyojulikana kama mpuzu, na [[nyumba]] zao ni za [[msonge]], [[udongo]] na miti, kulingana na sehemu mbalimbali, maana kuna sehemu zenye [[joto]] kama vile [[bonde]]<nowiki/>ni, na sehemu zenye [[baridi]] kama vile [[nyanda za juu]].
 
==Historia ya jina==
Historia ya Waha ilianzia katika [[kijiji]] kiitwacho Buha kilichopo Heru: hapo ndipo Waha walipofikia baada ya kutoka maeneo ya [[Burundi]], [[Rwanda]] na [[Kongo]].
 
Inafahamika kuwa Waha ni moja ya makabila kutoka Wabantu wa mashariki. Wabantu hao walipata kufika maeneo hayo hata kabla ya miaka ya 600 yaani kabla ya Wamanyema. Wamanyema na Waha ndio wenyeji wa Kigoma. Uenyeji huu tunaouzungumza ni miaka ya zamani sana: hata kabla ya kuanza kwa ukoloni hawa watu tayari walikuwa wakiishi pamoja na walikuwa wakipendana na kuthaminiana. Kuna vitu Waha waliwafundisha Wamanyema na pia kuna vitu Wamanyema waliwafundisha Waha na wote hawa waliipigania Tanganyika kutoka mikononi mwa serikali ya kikoloni. Hata mradi wa kuligawa [[bara]] la Afrika kati ya nchi kadhaa za [[Ulaya]] ulikuwa bado kabisa Wamanyema na Waha walikuwa wakiishi pamoja.
 
Ifahamike kuwa asilimia kubwa ya makabila mengi yaliyopo hapa Afrika yalipata majina kulingana na wageni walivyoelewa au walivyoona. Kuna makabila yaliyopata majina kutokana na namna wanavyopigana, yapo makabila yaliyopata majina namna wanavyopiga makelele na wengine walipewa majina kulingana na [[lugha]] yao au matamshi yao. Kwa upande wa kabila la Waha, ambao wanapatikana katika mkoa wa Kigoma, ukweli ni kwamba kabila hili ni miongoni mwa makabila ambayo yana historia kubwa sana tangu walipofika katika ardhi hiyo na pia ni kabila lenye umaarufu mkubwa nchini.
 
Kipindi watu hawa wanafika maeneo ya [[Afrika Mashariki]] hawakujulikana kama kabila la Ha na hawakuja wakiwa kundi moja. Bali walikuja kwa mtindo wa koo na kila [[ukoo]] ulikuwa na jina lake.
 
Koo zilizokuwa hapo zilipata kumiliki ardhi. cha msingi ni kwamba watu hao walifanikiwa kuitwa majina ya maeneo waliyokaa kutokana na [[mazingira]] yake. Kwa mfano kuna ukoo uliokaa sehemu zenye [[udongo]] (Bayungu) walijiita Wayungu na wale waliokaa sehemu za mwinuko (Heru) walijiita Wanyaheru. Lakini mpaka kufikia miaka ya 1800, koo hizo ziliungana na kuishi sehemu na kutawaliwa na [[chifu]] mmoja. Ndipo watu hao walipoanza kupata jina moja lililowatambulisha kwa wageni.
 
Sasa kwa nini watu hao waliitwa Waha? Hii ndiyo mitazamo iliyosimulia asili ya neno Waha au Ha.
 
1. Wapo waliodai kuwa asili ya neno Waha au Ha ni pale wageni walipofika katika ardhi ya Kigoma na kuwauliza watu hao kuwa “ninyi ni wakina nani” na ndipo watu hao walipojibu “tur; Abhaha” wakimaanisha "sisi ni wazaliwa wa hapa hapa". Hapo wageni hao walikariri kuwa Waha kwa kuchukua neno “ha”,,, Kiuhalisia Waha na Wamanyema ni watu wamoja: tangu enzi na enzi walipendana na kuthaminiana.
 
2. Wapo wanaodai kuwa wageni walipokuja na kukuta ufalme wa Buha umekua na ulikuwa na watu wengi, walimuuliza [[mfalme]] wao kuwa “hawa ni wakina nani”, na ndipo mfalme wa Buha alipojibu kuwa, “N’abhaha” akimaanisha kuwa “hawa ni wenyeji wa hapahapa” na hapo wageni hao walipata neno “Ha” na walipoandika waliaandika hivyo.
 
Maelezo hayo yalitolewa na watu waliokuwa wamekutwa katika ardhi ya Buha. Kwa upande mwingine, historia inafafanua kuwa, [[Watutsi|Watusi]] walikuwa watawala wa kabila la Waha na kuna mahusiano makubwa sana kati ya Watusi na Waha. Hivyo hata neno Waha bado lilionekana kuhusiana na Watusi.
 
Kwa Watusi neno Abaha lina maana ya mtu yeyote “anaowapa ardhi” na kwa Watusi aliyekuwa akitoa ardhi alifahamika kwa jina la Mtoke. Na mteko alikuwa akitoa ardhi kwa Watusi, walifahamika kwa jina moja la Uwaha.
 
Waliolima shamba moja na Mteko walijiita “Abhaha”, hata kuna baadhi ya Watusi hujiita “Waha” na ndiYo maana hata walivyotawala walijiita hivyo...
 
{{Makabila ya Tanzania}}