Ugonjwa wa Parkinson : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Ugonjwa wa Parkinson ([http://Parkinson's%20disease https://en.wikipedia.org/wiki/Parkinson%27s_disease]) ni ugonjwa wa kibongo ambapo mtu hukosa homoni ya dopa...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 08:10, 26 Septemba 2018

Ugonjwa wa Parkinson (https://en.wikipedia.org/wiki/Parkinson%27s_disease) ni ugonjwa wa kibongo ambapo mtu hukosa homoni ya dopamini. Hili hufanyika baada ya seli zinazotengeneza dopamini kuharibika. Dalili ya ugonjwa huu wa parkinson ni kutetemeka kwa mikono(hand tremors), pamoja na shida ya kutembea. Huenda pia mtu akawa na shida za kufikiria. Wagonjwa wa Parkinson huwa na huzuni, utomvu wa usingizi pamoja na wasiwasi mwingi.

Kiini cha Ugonjwa wa Parkinson

Haijulikani haswa kiini cha ugonjwa huu kutokea lakini yakisiwa kwamba hurithiwa kutoka kwa kizazi hadi kingine. Sababu za kimazingira huweza pia kuchangia ugonjwa huu kwa mfano yasemekana kwamba wanaofanya kazi za kupuliza kemikali kwa mimea huenda wakaupata kwa urahisi. Wanaume huwa kwa hatari kubwa kuupata ugonjwa huu kuliko wanawake.

Matitabu ya ugonjwa wa Parkinson

Kwa sasa, hamna matitabu ya kutibu ugonjwa huu lakini kuna dawa ambazo wagonjwa hupewa ili kudhibiti dalili za ugonjwa. Matibabu haya ni kama levodopa na sinemet. Dawa hizi hufanya kazi kwa muda fulani tu na baadaye huwa hazifanyi. Ifikapo kipindi hiki, wagonjwa hushauriwa kula vizuri na kufanya mazoezi ambayo husaidia pia kudhibiti ugonjwa.