Pango : Tofauti kati ya masahihisho

pango ,mwamba mkubwa ulio na mlango
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Kodi ya kupanga (lease au rent) ni pesa au mkataba unaoafikianwa na mwenye nyumba au ardhi na anayepanga mali hiyo. Kwa kawaida, kodi ya nyumba za kuishi au za...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 06:40, 27 Septemba 2018

Kodi ya kupanga (lease au rent) ni pesa au mkataba unaoafikianwa na mwenye nyumba au ardhi na anayepanga mali hiyo. Kwa kawaida, kodi ya nyumba za kuishi au za kibiashara hulipwa baada ya muda fulani ambao mwenye mali ile na anayekodi wamekubaliana. Kutolipa kodi ili huenda anayepanga akafurushwa nje au akachukuliwa hatua za kisheria kwa kutotimiza wajibu wake katika mkataba walioweka na mwenye nyumba. Mwenye mali kwa upande wake anafaa ahakikishe kwamba mahala pale pamefanyiwa ukarabati, anawajibika anapotakikana na mpangaji.

Sababu za kukodi au kupanga nyumba

  • Huenda anayekodi haana pesa za kununua nyumba yake au ardhi na kwa hivyo inambidi akodi.
  • Huenda ukawa unahitaji nyumba au ardhi kwa muda mfupi na kwa hivyo hamna maana ya kununua mali ile ikiwa kuna anayekodisha
  • Huenda mpangaji anataka kumwachia mwenye mali kazi za kurekebisha na kukarabati mali ile na kwa hivyo anaonelea heri asinunue bali akodishe
  • Huenda anayekodi akahofia kupata hasara kwa kununua kwani mali ile inaweza kushuka bei baada ya muda fulani kwa hivyo anaonelea heri akodishe kuliko kununua.

Maswala ibuka katika kodi

Hivi leo, biashara ya kukodisha mali imekuwa kubwa sana. Kulingana na Shelter Afrique, kikundi kinachojishughulisha na mambo ya makao mema kwa Waafrika, yakadiriwa kuwa kila mwaka nyumba bilioni mbili hutengenezwa kila mwaka na kukodishwa kwa watu. Mwakani 2016, walikadiri pia kuwa asilimia arobainne(40%) ya waafrika walikuwa wakiishi katika miji mikuu na kwa hivyo walihitaji kukodishiwa nyumba.

Kukodi ofisi za kazi

Watu wamekuwa wakikodi ofisi za kufanyia kazi kwa muda mrefu haswa katika miji ambapo wataweza kuwasiliana na wateja wao kwa urahisi. Hivi leo, kumekuwa na ofisi za kukodisha ambapo mpangaji hupata kuwa kila kitu kama samani, mtandao, simu, ukarabati wafanywa kwa ofisi yake. Anapohitajika ni kulipa tu kodi na aanze kufanya kazi kwa ile ofisi. Hatohitaji kununua fanicha, kuweka nyaya za umeme au za simu katika ofisi ile. Pia usafi wafanywa na mwenye nyumba. Mwenye biashara ya Office Saigon asema kuwa wapangaji ofisi hawataki kuchoka wakishinda wakipamba ofisi zao. Wataka wewe uwafanyie yote hayo.

Mtandao na kodi

Matumizi ya intaneti yamerahisisha utafutaji wa nyumba au ardhi za kukodisha. Wenye mali ya kukodisha wanaweka makala ya mali yao katika mitandao nao wapangaji wanaweza kuwasiliana na wenyewe kwa urahisi zaidi. Kulingana na utafiti uliofanywa na YouGov, asilimia sabini na sita (76%) wanaosaka mali ya kukodi wataangalia kwa mtandao kwanza kama mali wanayotafuta ipo