Mamluki : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Created by translating the page "Mercenary"
(Hakuna tofauti)

Pitio la 09:31, 12 Oktoba 2018

Mamluki ni askari aliyekodiwa ambaye hayuko katika kikosi cha jeshi la nchi.[1] Mamluki hushiriki katika vita kwa ajili ya pesa au malipo mengine badala ya siasa au uzalendo.  

Leonardo da Vinci's Profilo di jeshi kapteni antico, pia inajulikana kama il Condottiero, 1480. Condottiero maana ya "kiongozi wa mamluki" katika Italia wakati wa Mwishoni mwa Zama za Kati na Renaissance.

Historia

Afrika

Afrika Ya Kale

Katika Misri ya Kale, Ramesses II aliwatumia mamluki 11,000 katika vita. Medjay, wanajeshi wa kukodiwa kutoka Nubia, walihudumu pamoja na jeshi la Misri wakati wa Ufalme wa Kale wa Misri hadi Ufalme Upya wa Misri. Wapiganaji wengine walioajiriwa kutoka nje ya mipaka ya Misri ni pamoja na vikosi vya Walibya, Wasiria na Wakanani wakati wa Ufalme Upya na Washardana kutoka Sardinia ambao huonekana na helmeti maalum katika michoro, kama walinzi wa Ramesses II.[2] Watawala Wagiriki wa Misri ya Ptolemaio, walitumia mamluki Wakelti.[3] Karthago ilitegemea mamluki kupigana katika vita vyake.

Karne ya 19 na 20

 
Frederick Russell Burnham katika Afrika
Mgogoro Wa Kongo
 
Mamluki wazungu wakipigana bega kwa bega na vikosi vya Wakongo, mwaka 1964

Mgogoro wa Kongo wa mwaka 1960-1965 ulikuwa kipindi cha machafuko katika Jamhuri ya Kwanza ya Kongo ambayo iliundwa kwa kupewa uhuru na Ubelgiji na ikakatizwa baada ya Joseph Mobutu kuchukua madaraka ya nchi kwa mabavu. Katika kipindi hicho, mamluki walitumiwa na baadhi ya vikundi katika mgogoro na wakati mwingine, walitumiwa na Walinzi wa amani wa UM.

Katika miaka ya 1960 na 1961, Mike Hoare alikuwa mamluki aliyekuwa akiongoza kitengo cha wanajeshi waliokuwa wakiongea Kiingereza, kilichokuwa kikiitwa "4 Commando", kilichokuwa Katanga, mkoa ambao ulikuwa unajaribu kujitenga na Kongo ili uwe nchi huru chini ya uongozi wa Moise Tshombe. Hoare aliandika matukio hayo katika kitabu chake kiitwacho Road to Kalamata.

Katika mwaka wa 1964 Tshombe (aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kongo) alimwajiri Meja Hoare aongoze kitengo cha kijeshi kilichokuwa kikiitwa "5 Commando", kilichokuwa na wapiganaji 300, wengi ambao walikuwa wametoka Afrika Kusini. Lengo la 5 Commando lilikuwa kupigana na kikundi cha waasi, kilichokuwa kikiitwa Simba, ambacho kilikuwa kimetwaa karibu thuluthi mbili ya nchi.

Katika Operesheni Dragon Rouge, 5 Commando walishirikiana na wanajeshi Wabelgiji, marubani kutoka Kuba waliokuwa mahamishoni, na mamluki waliokuwa wameajiriwa na CIA. Lengo la Operesheni Joka Rouge lilikuwa kutwaa Stanleyville na kuokoa mamia ya raia (hasa Wazungu na wamisionari) ambao walikuwa mateka wa waasi wa Simba. Operesheni hiyo iliokoa maisha ya watu wengi;[4] hata hivyo, ilimchafulia sifa Moise Tshombe kwa kuwa iliwarudisha mamluki wazungu katika Kongo tu baada ya uhuru wa nchi. Ilikuwa mojawapo ya sababu za Tshombe kukosa msaada kutoka rais wa Kongo, Joseph Kasa-Vubu, ambaye alimpiga kalamu.

Wakati huo huo, Bob Denard aliongoza "6 Commando" na "Black Jack" Schramme aliamuru "10 Commando" na William "Rip" Robertson aliongoza kikosi cha Wakuba waliokuwa mahamishoni.[5]


Biafra

Mamluki walitumiwa kupigana katika vita vya wenyewe kwa wenyewe Nijeria, mwaka 1967-1970.[6] Wengine walitumiwa kuendesha ndege kwa niaba ya Wabiafra. Kwa mfano, Oktoba mwaka 1966,  ndege aina DC-4M Argonaut ya shirika la ndege la Burundi lililokuwa likiendeshwa na mamluki Heinrich Wartski, aliyejulikana pia kama Henry Wharton, lilianguka Kameruni likiwa na bidhaa za kijeshi zililzokuwa zikipelekwa Biafra.[7]

Mei mwaka 1969, Carl Gustaf von Rosen aliunda kikosi cha ndege tano zilizokuwa zinajulikana kama Watoto wa Biafra (ing: Babies of Biafra) zilizoshambulia na kuharibu ndege za Nijeria[8] na zikasambaza msaada wa chakula. 

Eritrea na Ethiopia

Nchi zote mbili ziliajiri mamluki katika Vita vya Eritrea na Ethiopia vilivyokuwa kati ya mwaka 1998 hadi 2000. Iliaminiwa kuwa mamluki kutoka Urusi walikuwa wakiendesha ndege za kivita za pande zote mbili.[9][10]



Marejeo

  1. Protocol Additional to the Geneva Conventions of 12 August 1949, and relating to the Protection of Victims of International Armed Conflicts (Protocol 1), Article 47. Iliwekwa mnamo 20 Apr 2018.
  2. Healy, Mark; New Kingdom Egypt;
  3. Rootsweb: Celts in Egypt. Archiver.rootsweb.ancestry.com (24 February 2004). Iliwekwa mnamo 17 October 2011.
  4. "Changing Guard", Time Magazine, 19 December 1965. Retrieved on 6 June 2007. 
  5. p.85 Villafaña, Frank Cold war in the Congo: The Confrontation of Cuban military forces, 1960–1967 Transaction Books
  6. The Mercenaries in Time Magazine 25 October 1968
  7. Tom Cooper Civil War in Nigeria (Biafra), 1967–1970 13 November 2003. Second paragraph.
  8. Gary Brecher. Biafra: Killer Cessnas and Crazy Swedes Archived 14 Januari 2008 at the Wayback Machine 15 October 2004.
  9. "Sentinel Security Assessment - North Africa, Air force (Eritrea), Air force", Jane's Information Group, 26 October 2011. 
  10. Africa News Online: "In defiance, Eritrea was born; in defiance, it will live forever." 30 May 2000.

Tanbihi

  • Guy Arnold. Mercenaries: The Scourge of the Third World. Palgrave Macmillan, 1999. ISBN 978-0-312-22203-1978-0-312-22203-1
  • Doug Brooks & Shawn Lee Rathgeber. "The Industry Role in Regulating Private Security Companies", Canadian Consortium on Human Security – Security Privatization: Challenges and Opportunities, Vol. 6.3, University of British Columbia, March 2008.
  • Niccolò Machiavelli. The Prince. 1532. Ch. 12.
  • Anthony Mockler. Hired Guns and Coups d'Etat: Mercenaries: Thirty Years 1976-2006. Hunter Mackay, 2007.
  • Anthony Mockler. The Mercenaries: The Men Who Fight for Profit—from the Free Companies of Feudal France to the White Adventurers in the Congo. Macmillan, 1969.
  • Anthony Mockler. The New Mercenaries: The History of the Mercenary from the Congo to the Seychelles. Paragon House, 1987.
  • Robert Young Pelton. Hunter Hammer and Heaven, Journeys to Three World's Gone Mad, ISBN 1-58574-416-61-58574-416-6
  • Jeremy Scahill. Blackwater: The Rise of the World's Most Powerful Mercenary Army, Nation Books, 2007. ISBN 1-56025-979-51-56025-979-5
  • Peter J. Woolley. "Soldiers of Fortune," The Common Review, v. 5, no. 4(2007), pp. 46–48. Review essay.