Kitabu cha Yeremia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Bot: Migrating 1 interwiki links, now provided by Wikidata on d:Q131590
No edit summary
Mstari 1:
[[File:Jeremiah lamenting.jpg|250px|right|thumbnail|Mchoro wa [[Rembrandt van Rijn]] unaomuonyesha "Yeremia Akililia Maangamizi ya Yerusalemu", mwaka [[1630]] hivi.]]
'''Kitabu cha [[nabii Yeremia]]''' ni kimojawapo kati ya [[vitabu vya kinabii]] vilivyo virefu zaidi katika [[Tanakh]] ([[Biblia ya Kiebrania]]), na kwa hiyo pia katika [[Agano la Kale]] ambalo ni sehemu ya kwanza ya [[Biblia ya Kikristo]].
 
Kama [[vitabu]] vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya [[ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].
 
==Wito na muda wa unabii wake==
Akiwa bado [[kijana]], [[kuhani]] huyo mpole aliitwa na Mungu awe [[nabii]] katika kipindi cha [[misukosuko]] huko [[Mashariki ya Kati]], ambapo [[Wakaldayo]] wa [[Babeli]] waliwashinda [[Waashuru]] na kueneza [[utawala]] wao hadi kuteketeza [[Yerusalemu]] na [[hekalu]] lake. Katikati ya matukio hayo yote, Yeremia alipewa kazi ngumu ya kuonya na kutisha watu wa [[Yuda]] kwa kutabiri maangamizi hayo ili wamrudie kweli Mungu wasipatwe na [[adhabu]] kali kama wenzao wa [[kaskazini]]. Lakini wao hawakuwa tayari kufanya hivyo, wakijiamini hawatakoma kwa kuwa, tofauti na hao, wanatawaliwa na [[ukoo]] halali wa [[Daudi]] ulioahidiwa kudumu [[milele]], tena wanatunza hekalu pekee la Mungu na [[sanduku la agano]] analokalia. Walidanganywa na ma[[nabii wa uongo]] waamini hivyo, kumbe walitakiwa kujirekebisha na kufuata kweli masharti ya [[agano]] lenyewe.
 
Hivyo [[nabii Yeremia]] alilazimika kupambana na wote: wafalme, makuhani na manabii wenzake, [[ndugu]] wa ukoo wake na wananchi kwa jumla. Ilimbidi ashindane nao kinyume cha [[silika]] yake ya [[upole]] iliyomfanya apende kuelewana na watu. [[Upweke]] wake ulizidiwa na [[useja]] alioitiwa na Mungu ili aonye hata kwa njia hiyo kwamba mambo yajayo ni magumu na ya kutisha hata iwe afadhali kutozaa watoto.
 
Katika miaka yote 40 na zaidi ya [[unabii]] wake kipindi kizuri ni miaka ile 13 tu ([[622 K.K.|622]] - [[609 K.K.]]) ambapo [[Yosia]] alifanya urekebisho wa kidini kuanzia Yerusalemu hadi kwa mabaki ya [[Waisraeli]] wa kaskazini, akizuia wote wasiabudu miungu mingine wala wasimtolee Mungu [[sadaka]] nje ya [[hekalu la Yerusalemu]]. Kipindi hicho mji mkuu wa Ashuru uliangamizwa alivyotabiri kwa furaha Nahumu (612 hivi K.K.).
Mstari 22:
 
===Sala yake (Yer 15:16)===
 
'Maneno yako yalionekana, nami nikayala;
na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu,
Line 29 ⟶ 28:
 
==Mwisho wa unabii wake==
 
Baada ya Yerusalemu kuteketezwa (587 K.K.) Yeremia alichagua kubaki nchini pamoja na mafukara badala ya kuhamia Babeli kwa [[heshima]] ya pekee (39:8-40:6), ila ukatokea uasi akalazimishwa na Waisraeli wenzake kuwafuata Misri: huko akawaonya wasifuate Upagani lakini wakakataa tena kumsikiliza (42-44).
 
Line 35 ⟶ 33:
 
==Nyongeza==
 
Kama nyongeza ya kitabu cha Yeremia tuna [[Maombolezo (Biblia)|Maombolezo]] matano juu ya Yerusalemu ulioteketezwa, ambamo inaonekana toba halisi baada ya tukio hilo. Hatujui yametungwa na nani.
 
==Viungo vya nje==
 
*[http://www.biblephone.net/mobile/index.php/swa/2/Jerem/ Kitabu cha Yeremia katika [[tafsiri]] ya [[Kiswahili]] (Union Version)]
* (Jewish Encyclopedia) [http://www.jewishencyclopedia.com/view.jsp?artid=225&letter=J&search=Jeremiah Book of Jeremiah article]
Line 54 ⟶ 50:
 
{{Biblia AK}}
{{mbegu-Biblia}}
 
[[Category:Vitabu vya Agano la Kale|Yeremia]]