Mwezi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 56:
Hata kama [[Warusi]] na Wamarekani walifikisha [[bendera]] zao mwezini, hakuna anayedai [[mali]] huko. Katika [[mkataba kuhusu anga za nje]] nchi 192 za dunia zimepatana ya kwamba mwezi utaangaliwa sawa na maeneo ya kimataifa ya [[bahari]]. Walipatana pia ya kwamba itakuwa marufuku kupeleka [[silaha]] kali kama [[bomu la nyuklia|za nyuklia]] angani. [[Taifa|Mataifa]] mengi ya dunia yamejiunga na [[mkataba]] huo, isipokuwa nchi chache hasa za [[Afrika]] hazikutia sahihi kama vile [[Tanzania]].
 
Lakini kuna watu binafsi wanaodai mali ya mwezi. Tangu mwaka 1980 yupo Mwamerika mmoja aliyefaulu kuandikisha Mwezi kwa jina lake kwenye ofisi ya msajili wa viwanda [[Mji|mjini]] [[San Francisco]] akiendelea kuuza hati za kumiliki maeneo mwezini. Kuna pia familia moja pale Ujerumani iliyorithi hati ambako mfalme wa Prussia kwenye mwaka 1756 alitoa zawadi ya Mwezi kwa mzee wao. Taasisi ya Sheria ya Anga za Nje ''(International Institute of Space Law)'' ilitoa tamko kuwa madai haya hayana msingi wa kisheria <ref>[http://www.iislweb.org/docs/IISL_Outer_Space_Treaty_Statement.pdf Statement by the Board of Directors of the International Institute of Space Law (IISL) on Claims to Property Rights Regarding the Moon and Other Celestial Bodies], International Institute of Space Law. 2004</ref>.
Lakini kuna watu binafsi wanaodai mali ya mwezi.
 
Kwanza kuna [[familia]] ya Jürgens wanaoishi Westerkappeln ([[Ujerumani]]) walipewa [[hati ya kumiliki]] mwezi na [[mfalme]] wa [[Prussia]] [[Friederich II]] tarehe [[15 Julai]] [[1756]] [[BK]]. Mfalme alitoa hati kama [[zawadi]] ya [[shukrani]] kwa [[huduma]] bora akiamuru ya kwamba Martin Jürgens atakuwa mwenye mwezi na haki hii itarithiwa na [[mtoto]] wa kwanza.
 
Bila shaka ilhali hakujua haki za mali za Mjerumani katika mwaka [[1980]] Mwamerika Dennis M. Hope alifika mbele ya [[msajili]] wa [[viwanda]] [[Mji|mjini]] [[San Francisco]] akidai mwezi ni wake. Kufuatana na [[sheria]] ya Marekani kiwanda ni mali ya mtu akiandikisha dai lake na katika muda wa miaka minane hakuna upingamizi dhidi ya dai lake. Kwa njia hii - iliyowahi kufaulu tayari [[karne]] zilizopita [[Wazungu]] walipojipatia [[Amerika ya Kaskazini]] (hakuna aliyepinga madai yao mbele ya msajili) - alipata hati ya kumiliki akijaribu kuuza sasa mwezi polepole.
 
== Vyanzo ==