Mwakanuru : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
'''Mwakanuru''' (au '''Mwaka wa nuru'''; kwa [[Kiingereza]]: "Light year" <ref>https://en.wikipedia.org/wiki/Light-year</ref>) ni [[kizio]] cha [[umbali]] kinachotumiwa katika [[fani]] ya [[astronomia]]. Ni kipimo cha umbali ambao [[mwanga]] umeusafiri kwa [[mwaka]] mmoja wa [[dunia]] (ulimwengu)yaani [[siku]] 365.25.<ref>[https://www.iau.org/public/themes/measuring/ Measuring the Universe The IAU and astronomical units], Tovuti ya [[Ukia]], iliangaliwa Julai 2017</ref>.
 
Msingi wa kipimo hiki ni [[kasi ya nuru]]. [[Nuru]] inatembea takriban [[kilomita]] 300,000 kwa [[sekunde]]. [[Idadi]] kamili ni [[mita]] 299,792,458 kwa sekunde moja. [[Mwezi]] wa dunia yetu una umbali na dunia yetu kama sekunde moja ya nuru au kilomita [[lakhi]] [[tatu]] na dunia.
 
Katika mwaka mmoja umbali huo unafika [[mita]] 9.461 &nbsp;×&nbsp;10<sup>15</sup>.
 
Kipimo hiki kinahitajika kutaja umbali kati ya [[nyota]] na [[nyota]] angani. Umbali huu umepimwa kuwa miaka ya nuru [[mia]], [[elfu]] au hata [[milioni]] kadhaa. Kutokana na [[ukubwa]] wa [[ulimwengu]] umbali katika anga ni kubwa sana. Nyota jirani kabisa na [[jua]] letu inaitwa [[Alpha Centauri]] umbali wake ni 4.2 miaka ya nuru maana yake nuru yake inahitaji zaidi ya miaka minne hadi imefika kwetu. Kwa maana nyingine tunaiona nyota hii jinsi ilivyoonekana miaka minne iliyopita.
 
==Angalia pia==
*[[Kizio astronomia]] - kipimo cha kutaja umbali kati ya Dunia na Jua
*[[Parsek]] - kipimo cha kutaja umbali mkubwa katika [[anga la nje]]
 
==Tanbihi==