Usafiri wa anga-nje : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Picha:Soyuz TMA-5 launch.jpg|thumbnail|Roketi ya Soyuz TMA-5 ilirushwa uwanja wa anga Baikonur nchini Kazakhstan mnamo 14 Oktoba 2004 kikibeba wanaanga 3 kwen...'
 
No edit summary
Mstari 1:
[[Picha:Soyuz TMA-5 launch.jpg|thumbnail|Roketi ya Soyuz TMA-5 ilirushwa uwanja wa anga Baikonur nchini Kazakhstan mnamo 14 Oktoba 2004 kikibeba wanaanga 3 kwenda ISS]]
[[Picha:ISS March 2009.jpg|thumbnail|Kituo cha anga cha Kimataifa ISS mnamo mwaka 2009]]
'''Usafiri wa anga la -nje''' ni kila aina za [[safari]] au usafiri inayofikia nje za [[angahewa]] ya [[Dunia]] kwenye [[anga la -nje]]. Ilhali hakuna mpaka kamili baina ya angahewa na anga la -nje kuna mapatano ya kutazama [[umbali]] wa [[kilomita]] 100 kama chanzo cha anga la -nje.
 
Chombo cha kwanza kilichofikia juu ya km 100 kilikuwa [[roketi]] ya Kijerumani aina ya [[V-2]] katika majaribio ya mwaka [[1944]].<ref>"The V2 and the German, Russian and American Rocket Program", C. Reuter. German Canadian Museum. p. 170. ISBN 1-894643-05-4, ISBN 978-1-894643-05-4</ref>
 
Chanzo cha usafiri wa anga la -nje kilikuwa kuruka kwa [[chombo cha angani]] cha [[Umoja wa Kisovyeti|Kisovyieti]] [[Sputnik 1]] mnamo [[4 Oktoba]] [[1957]] iliyokuwa [[satelaiti]] ya kwanza iliyozunguka Dunia angani.
 
[[Kiumbehai]] wa kwanza aliyefikishwa hadi anga la -nje alikuwa [[mbwa]] [[Laika]] kwa njia ya satelaiti ya [[Sputnik 2]]. [[Mtu]] wa kwanza katika anga la -nje alikuwa [[Mrusi]] [[Yuri Gagarin]] aliyezunguka Dunia mara moja tarehe [[12 Aprili]] [[1961]] kwa [[Vostok 1]].
 
[[Marekani]] ilifaulu kupeleka watu wa kwanza hadi uso wa [[Mwezi (gimba la angani)|mwezi]] tarehe [[20 Julai]] [[1969]]: hao walikuwa [[Neil Armstrong]] na [[Buzz Aldrin]].
 
Tangu mwaka [[1986]] Umoja wa Kisovyeti ilianza kujenga [[kituo cha angani]] [[MIR]] kilichofuatwa na [[Kituo cha Anga cha Kimataifa ISS]] tangu [[1998]]. Katika vituo hivyo [[wanaanga]] na [[wanasayansi]] kutoka nchi mbalimbali waliweza kukaa angani kwa miezi na kufanya [[utafiti]] wa [[mazingira]] ya anga la -nje.
 
Usafiri wa anga la waanga-nje umeendelea kwa kupeleka [[vyombo vya angani]] hadi [[sayari]] nyingine. Shabaha ya safari hizi ni [[upelelezi]] na utafiti wa kisayansi. [[Voyager 1]] ni chombo cha kwanza kilichotoka katika [[mfumo wa jua]] letu mnamo mwaka [[2012]].
 
Katika mazingira ya karibu zaidi ya Dunia kuna satelaiti nyingi zinazozunguka sayari yetu na kutekeleza [[kazi]] hata za [[biashara|kibiashara]] kama vile [[upimaji]] wa [[hali ya hewa]], kurusha [[programu]] za [[runinga]] na [[redio]], kutuma [[data]] za [[GPS]] au za [[simu]].
Line 20 ⟶ 19:
{{reflist}}
 
[[Category:Usafiri wa anga la -nje|* ]]
[[Jamii:Teknolojia]]
[[Jamii:Astronomia]]