Nyota nova : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 3:
 
==Historia ya utazamaji==
Zamani nyota zote zilizowaka hivi ziliitwa kwa jina lilelile "nova". Jina hili lilitumiwa mara ya kwanza na [[Tycho Brahe]] ambaye katika mwaka 1572 aliona nyota mpya katika eneo la kundinyota [[Mke wa Kurusi|Mke wa Kurusi ''(Cassiopeia)'']] na kueleza utafiti wake katika kitabu cha "De stella nova"(Kuhusu nyota mpya) <ref>Kilatini kwa "Kuhusu nyota mpya", linganisha [https://www.nasa.gov/mission_pages/WISE/multimedia/gallery/pia13119.html Tycho's Supernova Remnant], tovuti ya NASA, iliangaliwa Februari 2108</ref>. Wakati huo Tycho Brahe alianzisha majadiliano kuhusu mafundisho ya wataalamu wa kale walioamini kwamba hakuna mabadiliko yoyote kwenye anga ya nyota<ref>Majadiliani yaliendelezwa na [[Johannes Kepler]] aliyeandika mwaka 1606 pia kuhusu "Stella Nova in pede Sagitarii" (kuhusu nyota mpya mguuni pa kundinyota Kausi)</ref>.
 
Hata kabla ya Tycho kulikuwa na taarifa kuhusu nyota zilizotokea angani. Taarifa ya kale zaidi ni ya wanaastronomia nchini China kwenye mwaka 185 baada ya Kristo kuhusu "nyota geni" iliyoonekana karibu na [[Rijili Kantori|Rijili Kantori ''(α Centauri)'']]. Nova nyingine ilitazamiwa mwaka 1006 na kurekodiwa na wanaastronomia Wachina, Wajapani na Wakristo wa Baghdad. Mabaki yake huonekana hadi leo kama "Nebula ya Kaa" katika eneo la [[Tauri (kundinyota)|Tauri ''(Taurus)'']].
Mstari 15:
==Tabia za nova==
[[Picha:Making a Nova.jpg|300px|thumb|Nyota Kibete Cheupe inavuta mata kutoka Jitu Jekundu jirani kwake.]]
Nyota nova za kawaida zinatokea katika [[Nyota pacha|mfumo wa nyota pacha]]. Nadharia inayokubalika na wengi inasema: [[nyota kibete cheupe]] na nyota kubwa, hasa [[jitu jekundu]], zinazungukana kwa umbali wa karibu. Kibete cheupe kimeshamaliza [[hidrojeni]] yake na kujikaza, hivyo [[graviti]] yake bado ni kubwa ingawa mjao wake ni mdogo, pia niina joto sana. Jitu jekundu la jirani linaendelea kupanuka. Hapa sehemu ya mata ya tabaka za nje ya nyota kubwa inavutwa na graviti ya nyota ndogo na kuhamia upande wake. Sehemu ya mata hii ni hidrojeni inayokusanyika kwa umbo la [[diski ya uongezekaji]]<ref>ing. "accretion disk"</ref> inayozunguka Kibete Cheupe na hatimaye kufikia karibu zaidi na kuunda angahewa. Hidrojeni hii inapashwa moto na uso wa Kibete Cheupe hadi kufikia halijoto ya kutosha ya kuanzisha [[myeyungano wa kinyuklia]] ''(nuclear fusion)''.
 
Mchakato huu unazalisha kiasi kikubwa cha nishati na kurusha sehemu ya hidrojeni inayowaka kwenye anga laya nje. Hii inaongeza mwangaza wa nyota inayoonekana sasa kama nyota nova. Kiasi cha masi inayorushwa angani wakati wa kuwaka inalingana takriban na <sup>1</sup>/<sub>10,000</sub> ya [[masi ya Jua]].
 
Maendeleo ya nova inafuata hatua kama hizi:
Mstari 28:
 
==Kugunduliwa kwa nova==
Kila mwaka kuna takriban nyota nova 10 zinazotazamwa katika Njia Nyeupe<ref>[http://cbat.eps.harvard.edu/nova_list.html List of Novae in the Milky Way], tovuti ya Central Bureau for Astronomical Telegrams, iliangaliwa Februari 2018</ref>. Lakini wanaastronomia hukadiria kwamba idadi halisi ni kubwa zaidi, labda mnamotakribani 50 zinazotokea kila mwaka katika galaksi yetu<ref>[https://arxiv.org/pdf/1606.02358.pdf Shafter, A.W. (January 2017). "The Galactic Nova Rate Revisited". The Astrophysical Journal. 834 (2): 192–203]</ref>.
 
Nyota nova zinagunduliwa pia katika galaksi nyingine, kwa mfano katika [[galaksi ya Andromeda]] (M31) na penginepo<ref>[http://cbat.eps.harvard.edu/CBAT_M31.html M31 (Apparent) Novae Page], tovuti ya Central Bureau for Astronomical Telegrams, iliangaliwa Februari 2018 </ref>.
 
==Nova za kurudia==
Kinadharia mchakato huu unaweza kurudia mara kadhaa kwa sababu baada ya mlipuko wa angahewa ya nyota ndogo, mata kutoka jirani mkubwa inaanza kuvutwa tena. Nyota RS Ophiuchi katika [[Hawaa (kundinyota)|kundinyota ya Hawaa]] ilitazamwa kuwaka mara sita<ref>[https://www.aanda.org/articles/aa/full_html/2009/15/aa11417-08/aa11417-08.html Brandi, E.; Quiroga, C.; Mikołajewska, J. (2009). "Spectroscopic orbits and variations of RS Ophiuchi". Astronomy and Astrophysics. 497]</ref>: 1898, 1933, 1958, 1967, 1985 na 2006.
 
Hadi sasa kuna nyota nova 10 zilizotazamwa kuwaka tena kati ya takriban 400 zilizogunduliwa katika [[Njia Nyeupe]]<ref>[http://iopscience.iop.org/article/10.1088/0004-637X/746/1/61/pdf M. J. Darnley, V. A. R. M. Ribeiro1,2, M. F. Bode, R. A. Hounsell, and R. P. Williams, ON THE PROGENITORS OF GALACTIC NOVAE], The Astrophysical Journal, Volume 746, Number 1, Published 2012 January 25 </ref>; kwa hiyo hakuna uhakika bado kuhusu muda wa kawaida uliopo baina ya kuwaka kwa nyota. Kama nyota kibete imeendelea kukusanya mata nyingi kuna uwezekano kwamba inalipuka mwishoni kama supanova <ref>Sababu yake ni ya kwamba graviti yake inaweza kuzidi shinikizo ya mnururisho ndani yake ambayo kwa kawaida inatunza uwiano ndani ya nyota</ref>