Jua : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 19:
 
==Mnururisho na upepo wa Jua==
Jua linatoa [[mwanga]], [[joto]] na [[mnururisho]] mwingine wa aina mbalimbali. Sehemu ya mnururisho huu unatoka kwa umbo la vyembechembe kama protoni na elektroni ambazo kwa jumla hujulikana pia kama [[upepo wa Jua]]. Masi ya upepo wa Jua ni takriban tani moja kwa kila sekunde.<ref>Carroll, Bradley W.; Ostlie, Dale A. (1995). An Introduction to Modern Astrophysics (revised 2nd ed.). Benjamin Cummings. p. 409. ISBN 0-201-54730-9.</ref> [[Asili]] ya [[nishati]] hii ni mchakato wa [[myeyungano wa kinyuklia]] ndani yake. Katika myeyungano huo hidrojeni inabadilishwa kuwa heliheliamu. Elementi nyingine zinatokea pia kwa kiasi kidogo. Badiliko kutoka hidrojeni kwenda heliheliamu inaachisha nishati inayotoka kwenye Jua kwa njia ya mnururisho.
 
[[Nishati]] ya mnururisho huu ni msingi wa maisha ya [[mmea|mimea]] na [[kiumbehai|viumbe hai]] katika dunia. Nuru ya Jua inabadilishwa na mimea kwa njia ya [[usanisinuru]] kuwa [[nishati ya kikemia]] inayojenga [[miili]] yao itakayokuwa [[lishe]] tena ya mimea na wanyama.