Chuo cha Kikristo cha Aleksandria : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa umeelekezwa kwenda Shule ya Aleksandria
Tag: New redirect
Removed redirect to Shule ya Aleksandria
Tag: Removed redirect
Mstari 1:
'''Chuo cha Kikristo cha [[Aleksandria]]''' (au ''Shule ya Elimu ya Kikristo ya Aleksandria'') katika [[karne]] za kwanza [[BK]] kilikuwa kimojawapo kati ya vituo vikuu viwili vya [[elimu ya Kikristo]] na kati ya [[vyuo]] vya kwanza vilivyofundisha [[imani]] ya [[Kikristo]] kwa namna ya kitaalamu. Wakati wa [[Mababu wa Kanisa]] [[teolojia]] na [[ufafanuzi]] wa [[Biblia ya Kikristo]] vilivyotolewa huko vilitofautiana na [[Shule ya Antiokia]]. [[jina|Majina]] ya vituo vyote viwili yalitokana na [[Jiji|majiji]] vilipostawi katika [[Ukristo]].
#REDIRECT[[shule ya Aleksandria]]
 
Wakati [[wanateolojia]] wa [[Antiokia]] ya [[Siria]] (leo nchini [[Uturuki]]) walifuata zaidi maneno yenyewe ya Biblia, wale wa [[Aleksandria]] ([[Misri]]) walipenda zaidi kuifafanua kiroho. Matokeo ya tofauti hizo yalijitokeza katika teolojia kuhusu [[fumbo]] la [[Yesu Kristo]] yakasababisha mafarakano makubwa ya [[karne ya 5]].<ref>Cross, F. L., ed. The Oxford Dictionary of the Christian Church. New York: Oxford University Press. 2005</ref>
 
Kadiri ya [[Jeromu]] shule ya Aleksandria ilianzishwa na [[Mwinjili Marko]]. Baadaye anatajwa [[Athenagora wa Athene]] ([[176]]), lakini kwa hakika zaidi [[Panteno]] [[181]], aliyeacha [[uongozi]] kwa [[mwanafunzi]] wake bora, [[Klementi wa Aleksandria]] mwaka [[190]].<ref>Cross, F.L.; Livingstone, E.A., eds. (1974). "Clement of Alexandria, St.". The Oxford Dictionary of the Christian Church (2 ed.). Oxford: Oxford University Press.</ref>Huyo alifuatwa na [[Origene]] akiwa na [[umri]] wa miaka 18 tu, na wataalamu wengine wanaoheshimiwa kama watakatifu katika [[Kanisa la Kiorthodoksi]] na [[Kanisa Katoliki]] kama [[Gregori Mtendamiujiza]], [[Heraklas]], [[Dionisi wa Aleksandria]] na [[Didimo Kipofu]].
 
Ilipoanzishwa kusudi lake lilikuwa kuwaelimisha [[Wapagani]] waliotafuta habari za imani mpya ya Kikristo kabla ya [[ubatizo]]. Chuo cha Aleksandria kikaendelea haraka kuwa [[kitovu]] cha elimu ya Kikristo na [[majadiliano]] kati ya imani ya Kikristo na [[falsafa]] ya Kigiriki iliyostawi sana Aleksandria, [[mji mkuu]] wa [[Misri]] wakati huo.
 
Ni kwamba kabla ya Misri kutwaliwa na [[Dola la Roma]] [[wafalme]] [[Watolemayo]] wa Misri waliwahi kuunda [[maktaba]] maarufu ambayo huaminiwa kuwa wakati wake ilikuwa maktaba kubwa zaidi [[duniani]] yenye [[vitabu]] 700,000. Kwa hakika ilikuwa maktaba kubwa kote [[Afrika]], [[Ulaya]] na [[Asia ya Magharibi]]. Hii ilikuwa na [[thamani]] kubwa kupita kiasi wakati ambako vitabu viliandikwa na kunakiliwa kwa [[mkono]] tu, na hivyo kuwa haba. Aleksandria ilikuwa [[kitovu]] cha [[elimu]] na [[uchunguzi]] wa kitaalamu duniani.
 
Chuo kikastawi mwanzoni katika vipindi ambako [[Wakristo]] hawakuteswa katika Misri, kikaona matatizo mazito wakati wa [[madhulumu]].
 
Tangu mwaka [[311]] [[uhuru wa dini]] ulitangazwa na [[Kaisari]] [[Konstantino Mkuu]] katika Dola la Roma na mateso ya Wakristo yalikwisha.
 
Chuo cha Aleksandria kikaendelea kutembelewa na wataalamu Wakristo kutoka pande zote za nchi za kandokando ya [[Mediteranea]], kwa mfano [[Basili Mkuu|Basili]] na Jeromu.
 
Kilibomolewa katika fujo zilizofuata [[Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli]] ([[381]]).
 
==Tazama pia==
#REDIRECT* [[shuleShule ya Aleksandria]]
 
==Tanbihi==
{{Reflist}}
 
{{mbegu-Ukristo}}
[[category:Misri]]
[[Category:Historia ya Kanisa]]
[[Category:Teolojia]]
[[Jamii:Mababu wa Kanisa]]
[[Category:Waorthodoksi wa Mashariki]]