Joseph Kamaru : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'Joseph Kamaru aliyezaliwa mwaka wa 1939 na kufariki mwezi wa Oktoba tarehe 3 mwaka wa 2018 alikuwa mwanamuziki wa benga na pia nyimbo za k...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 11:10, 30 Desemba 2018

Joseph Kamaru aliyezaliwa mwaka wa 1939 na kufariki mwezi wa Oktoba tarehe 3 mwaka wa 2018 alikuwa mwanamuziki wa benga na pia nyimbo za kumsifu Mungu. Kamaru alikuwa mtunzi mahiri aliyeweza kutunga nyimbo nyingi na kuuza takribani rekodi nusu milioni. Nyimbo zake zilikuwa na maudhui ya mapenzi, jinsi ya kuishi vizuri, kuhusu watoto kutumiwa vibaya kimapenzi na wazee pamoja na kuwakashifu wanasiasa.

Utoto wake

Kamaru wa Wanjiru kama alivyopenda kujiita alizaliwa Kangema, Muranga. Mwakani 1957, alihamia Nairobi alipopata kazi ya utopasi. Pia alifanya kazi ya nyumba iliyomwezesha kununa gitaa ya kwanza. Alianza kufuatilia ndoto yake ya muziki mwakani 1965.

Kazi ya muziki

Wimbo wa Kamaru wa kwanza uliovuma sana ni Celina aliouimba na dadaye. Nyimbo zake nyingi zilikuwa na jumbe za siasa na aliweza kuwa na mkabala mzuri na rais wa kwanza wa Kenya. Hata hivyo, walitofautiana alipouliwa Josiah Mwangi Kariuki (JM) na Kamaru akautoa wimbo wa kukaripia kitendo kile.

Kamaru pia walikua na mkabala mwema na rais wa pili Daniel Toroitich Arap Moi na aliweza kutunga wimbo kwa jina 'Safari ya Japani' baada ya kuzuru nchi ile na Moi mwakani 1980.

Ugonjwa na kufariki

Kamaru alifariki tarehe 3 mwezi wa Oktoba 2018 baada ya kuugua ugonjwa wa Parkinson. Alifariki akiwa na umri wa miaka 79.