Doreen Kessy : Tofauti kati ya masahihisho

Meneja wa uendeshaji
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ' '''Doreen Kessy''' ni mkuu wa operesheni katika kampuni ya Ubongo ,inayojihusisha na utoaji wa elimu kwa njia ya katuni. .<ref> http://vfhug.org/wp-content/u...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 11:04, 7 Machi 2019

Doreen Kessy ni mkuu wa operesheni katika kampuni ya Ubongo ,inayojihusisha na utoaji wa elimu kwa njia ya katuni. .[1] Doreen pamoja na wenzake watano ,waasisi wa kampuni ya ubongo ,waliamua kuanzisha ubongo ili kutoa mchango wao katika kupunguza tatizo la ukosefu au ueneaji wa elimu kwa watoto barani Afrika.[2].wanaamini kuwa kwa kutumia katuni hizi zitatoa mchango mkubwa katika kuwaelewesha watoto hivyo kuwapunguzia kazi kubwa walimu. .[3] Inakadiliwa kuwa familia 6.4 milioni katika nchi 31 Afrika wanatazama na kujifunza kutokana na Katuni za Ubongo kids kila wiki. [4]

Kazi

Kabla ya kuanzisha na kufanya kazi katika kampuni ya ubongo ,Doreen aliwahi pia kufanya kazi katika mashirika ya International Justice Mission ,Wells Fargo and Smile Africa na pia aliweza kubuni programu za kupunguza umaskini,ambazo zinatumika nchini Zimbabwe na Zambia. [5]


Elimu Yake

Doreen ana shahada ya uzamili ya biashara na utawala pia ana shahada ya kimataifa ya biashara na uchumi kutoka katika chuo kikuu cha Liberty kilichopo Virginia marekani. [6]

Uanaharakati

Ni mwanaharakati wa Elimu ,ambaye anajaribu kuleta mapinduzi katika Elimu kwa watoto wa Afrika,kufanya masomo yenye dhana kuwa ni magumu kwa kuyafundisha kwa njia ya katuini ili wanafunzi waweze kuyapenda na kuelewa kwa urahisi. .[7] Ameshiriki pia kama mmoja wa waigizaji ,kwa kuigiza sauti ya Kiingereza ya Ngedere katika katuni za Ubongo kids. .[8]

Tuzo

Kessy,ni miongoni mwa wavumbuzi 8 walio tunukiwa tuzo katika tuzo za Elimu zilizo kuwa zikitolewa na Umoja wa Afrika(the AU Education Innovation Prizes), Dakar, Senegal, 10 Oktoba 2018.[9]

Marejeo

  1. http://vfhug.org/wp-content/uploads/2018/01/Bios-of-Acumen-East-Africa-Fellows-for-2018-Cohort.pdf
  2. http://www.finland.or.tz/public/default.aspx?contentid=336675&contentlan=2&culture=en-US
  3. https://www.forbes.com/sites/ehrlichfu/2015/08/01/educating-kids-across-africa-through-a-local-cartoon-show/#1a587b6a237a
  4. https://www.weforum.org/agenda/2018/08/young-global-leaders-youth-day/
  5. https://www.crunchbase.com/person/doreen-kessy#section-overview
  6. https://www.crunchbase.com/person/doreen-kessy#section-overview
  7. http://vfhug.org/wp-content/uploads/2018/01/Bios-of-Acumen-East-Africa-Fellows-for-2018-Cohort.pdf
  8. http://vfhug.org/wp-content/uploads/2018/01/Bios-of-Acumen-East-Africa-Fellows-for-2018-Cohort.pdf
  9. https://au.int/en/pressreleases/20181010/ten-innovators-pitch-au-education-innovation-prizes