Umemenuru : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
 
Mstari 1:
'''Umemenuru''' (pia: '''umeme-mwanga''', '''fotovoltaiki''', ing.kutoka [[Kiingereza]] ''photovoltaics, photoelectricity'') ni [[umeme]] unaopatikana kutokana na [[nishati]] ya [[nuru]] hasa au kwa jumla kila aina ya [[mnururisho wa sumakuumeme]]. Badiliko hili linatokea katika [[seli]] zinazojulikana mara nyingi kama [[seli za sola]]. Seli ya umemenuru inatoa [[Mkondo wa umeme|mkondo]] wa takriban [[nusu]] [[volti]].
 
Nishati ya nuru ikikuta [[semikonda|mata yenye tabia ya nusukipitishi (semikonda)]] inasababisha mwendo wa [[elektroni]] ndani yake. Nuru inaundwa na vipande vidogo vinavyoitwa [[fotoni]]. Nishati ya fotoni ikigonga [[elektroni]] inaweza kuiondoa katika nafasi yake kwenye [[mzingo elektroni]] na kusababisha kutokea kwa [[mkondo wa umeme]].
 
Matumizi ya umemenuru yanapatikana katika [[umemejua|teknolojia ya umemejua]] kwa [[uzalishaji]] wa umeme, lakini pia kwa [[vihisio]] ''(sensor)'' vya aina nyingi kwa, mfano katika [[kamera]] au [[vifaa]] vya kupimakupimia [[umbali]], [[mwendo]] na kadhalika.
 
==Marejeo==
<references/>
 
==Viungo vya Njenje==
*[https://science.nasa.gov/science-news/science-at-nasa/2002/solarcells/ What is Photovoltaics?], tovuti ya NASA, iliangaliwa Machi 2019
 
*[https://dtpev.de/storage/app/uploads/intranet/public/5a2/faa/50f/5a2faa50f0887920056105.pdf Godwin Msigwa: Mafunzo ya umeme wa jua] , tovuti ya dtpev.de, iliangaliwa Machi 2019
 
*[https://www.livescience.com/41995-how-do-solar-panels-work.html How do solar panels work?], tovuti ya livescience.com, imeangaliwa Machi 2019
 
*[https://www.nrel.gov/docs/legosti/old/1448.pdf Basic Photovoltaic Principles and Methods], tovuti ya National Renewable Energy Laboratory, Marekani, iliangaliwa Machi 2019
 
{{mbegu-fizikia}}
 
[[jamii:umeme]]