Tofauti kati ya marekesbisho "Antara"

60 bytes added ,  miaka 2 iliyopita
no edit summary
[[Picha:Akarabu_Nge_Scorpius.png|400px|thumb|Antara (Antares) katika kundinyota yake ya Akarabu (pia: Nge) – Scorpius jinsi inavyoonekana kwa mtazamaji wa Afrika ya Mashariki]]
[[Picha: Nyota jitu kuu na jitu.png|400px|thumb|Ulinganifu wa ukubwa baina ya Antares (Antara), Simaki (Arcturus9 na Jua]]
'''Antara''' (kwa [[ing.Kiingereza]] na [[lat.Kilatini]] '''Antares'''; pia '''<big>α</big> Alpha&nbsp;Scorpii''', kifupi '''Alpha Sco''', '''α&nbsp;Sco''') ni [[nyota]] angavu zaidi katika [[kundinyota]] yala [[Nge (kundinyota)|Nge (pia: Akarabu)]] (''[[:en:Scorpius (constellation)|Scorpius]]''). Ni pia nyota angavu ya 15 kwenye [[anga]] yala [[usiku]]. [[Mwangaza unaoonekana]] unacheza kati ya mag 0.75 na 0.95.
 
==Jina==
Antara ilijulikana kwa [[mabaharia]] [[Waswahili]] tangu miaka mingi wakifuata njia yao [[Bahari|baharini]] wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. <ref>ling. Knappert 1993</ref>. Walipokea jina hili kutoka kwa [[Waarabu]] waliosema <big> عنترة </big> ''antarah'', ingawa leo wanatumia zaidi <big>قلب العقرب</big> ''qalb al-aqrab'' (moyo wa akarabu - nge). Hii „Antara“ ilikuwa namna ya kutamka jina la Ἄντάρης ''an-ta-res'' walilokuta kwa [[Klaudio Ptolemaio]] katika kitabu cha [[Almagesti]]<ref>Toomer, Ptolemy’s Almagest, p. 372 </ref>. Lakini Waarabu walichukua maana yake kwa kumtaja Antara ibn Shaddad (ar. عنترة بن شداد ) aliyejulikana kwao kama mshairi na shujaa wa Uarabuni wa Kale kabla ya Uislamu. Ἄντάρης - Antares iliyotumiwa na Ptolemaio inamaanisha "sawa na Ares", ilhali "Ares" ni jina la Kigiriki kwa mungu wa vita (kama Kiroma [[Mars]]) na pia jina la [[sayari]] ya nne katika [[mfumo wa Jua]] yaani [[Mirihi]]. Sawa na Mirihi pia Antara inaonekana kuwa na rangi nyekundu kwa macho matupu; mwangaza unafanana pia hivyo si vigumu kuchanganya nyota na sayari hii..
 
Kwa matumizi ya kimataifa Umoja wa Kimataifa wa Astronomia ulifuata mapokeo ya Kigiriki na kuorodhesha nyota hii kwa jina la "Antares" <ref>[https://www.iau.org/public/themes/naming_stars/ Naming Stars], tovuti ya [[Umoja wa Kimataifa wa Astronomia]] (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017</ref>.
Antara - Antares ni [[nyota badilifu]] na [[mwangaza unaoonekana]] wake unabadilika kati ya Vmag +0.6 na +1.6. [[Mwangaza halisi]] ni -5.3. Hivyo no nyota angavu ya 15 kwenye anga ya usiku.
 
Antara iko kwakatika umbali na [[Dunia]] wa [[miaka ya nuru]] 550 – 600. [[Masi]] yake ni takriban [[M☉]] 15 na nusukipenyo chake [[R☉]] 680 (vizio vya kulinganisha na Jua letu) . <ref> Schröder, K.-P.; Cuntz, M. (April 2007) </ref><ref>Ohnaka, K; Hofmann, K.-H; Schertl, D; Weigelt, G; Baffa, C; Chelli, A; Petrov, R; Robbe-Dubois, S (2013</ref>).
 
Ni [[nyota jitu kuu jekundu]] katika [[kundi la spektra]] M1.5 Iab-b. Inaitwa jitu kuu kwa sababu masi yake ni kubwa vile, mara 15 ya Jua. Ikiwa ni nyota jitu kuu jekundu ni nyota iliyopanuka baada ya kuishiakuishiwa [[hidrojeni]] katika [[kitovu]] chake; katika hali hii kitovu cha nyota kinajikaza na myeyungano wa hidrojeni unahamia kwenye tabaka za nje za nyota. Hii inasababisha kupanuka kwa nyota na kuongezeka kwa mwangaza wake. Kama Antara ingechukua nafasi ya Jua letu, sayari za [[Utaridi]], Zuhura, Dunia na Mirihi zingemezwa nayo maana kipenyo chake kinazidi obiti ya Mirihi.
 
Antara ina nyota msindikizaji kwa hiyo iki katika mfumo wa nyota pacha. Nyota hii ya pili huitwa α Scorpii B. Ni ndogo kuliko α Scorpii A yaani Antara ikiwa na masi ya [[M☉]] 7 na nusukipenyo cha [[R☉]] 5<ref>Kudritzki, R. P.; Reimers, D. (1978)</ref> . Ni [[nyota za safu kuu|nyota ya safu kuu]] ikiwa katika [[kundi la spektra]] B2. Kutokana na mwangaza mkubwa wa Antara yenyewe si rahisi kuiona iligunduliwa wakati Mwezi ulipita mbele ya nyota kuu na kuifunika.
==Tanbihi==
<references/>
 
==Viungo vya Nje==
* [http://www.constellation-guide.com/constellation-list/scorpius-constellation/ Constellation Guide: Scorpius]
*[http://stars.astro.illinois.edu/sow/Antares.html Antares (Alpha Scorpii), "Stars"], kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
* [http://www.ianridpath.com/startales/scorpius.htm Star Tales – Scorpius], tovuti ya Ian Ridpath, iliangaliwa Oktoba 2017
* [http://www.allthesky.com/constellations/scorpius/constell.html The Deep Photographic Guide to the Constellations: Scorpius]
 
==Marejeo==
 
* Allen, Richard Hinckley: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, ukurasa 59 ([https://ia801402.us.archive.org/14/items/starnamesandthe00allegoog/starnamesandthe00allegoog.pdf online kwenye archive.org])
*Knappert, Jan: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331
* Schröder, K.-P.; Cuntz, M. (April 2007), "A critical test of empirical mass loss formulas applied to individual giants and supergiants", Astronomy and Astrophysics, 465 (2): 593–601 [https://arxiv.org/pdf/astro-ph/0702172.pdf online hapa]
 
==Viungo vya Nje==
* [http://www.constellation-guide.com/constellation-list/scorpius-constellation/ Constellation Guide: Scorpius]
*[http://stars.astro.illinois.edu/sow/Antares.html Antares (Alpha Scorpii), "Stars"], kwenye tovuti ya Prof Jim Kaler, University of Illinois, iliangaliwa Oktoba 2017
* [http://www.ianridpath.com/startales/scorpius.htm Star Tales – Scorpius], tovuti ya Ian Ridpath, iliangaliwa Oktoba 2017
* [http://www.allthesky.com/constellations/scorpius/constell.html The Deep Photographic Guide to the Constellations: Scorpius]
 
[[Jamii:Nyota]]