Ozoni : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
 
Mstari 1:
'''Ozoni''' (ing.kwa [[Kiingereza]]: ''ozone'', pia ''trioxygen'') ni [[molekuli]] yenye [[alama]] ya O<sub>3</sub> inayofanywa na [[atomi]] [[tatu]] za [[oksijeni]].
 
==Tabia==
Inaonekana kama [[gesi]] ya [[buluu]] yenye [[harufu]] kali. Inatokea katika [[Tabaka|matabaka]] ya juu ya [[angahewa]] pale ambako [[urujuanimno|mnururisho wa urujuanimno]] unapasua molekuli za O<sub>2</sub>.
:<math>\mathrm{3 \; O_2 \longrightarrow 2 \; O_3}</math>
 
Inatokea pia katika [[mazingira]] ya [[mashine]] kama ya [[fotokopi]] zinazotumia [[volteji]] ya juu.
 
Si molekuli thabiti, inaachanahivyo inasambaratika tena baada ya [[muda]].
 
==Tabaka la ozoni==
Ozoni hupatikana kwa viwango vidogo vya [[ppm]] 0.6 katika angahewa. Kiasi kikubwa kipo kwenye [[tabakastrato]] baina ya [[kilomita]] 10 hadi 50 juu ya uso wa ardhi. Tabaka hili lenye ozoni linafyonza [[asilimia]] kubwa ya [[urujuanimno|mnururisho wa urujuanimno]] (asilimia 93-99[[%]]) ulio hatari kwa [[viumbehai]] [[duniani]].
 
==Athari kwa viumbehai==
Katika matabaka ya chini ya angahewa ozoni ni [[sumu]] kwa viumbehai ikitokea kwa viwango juu ya ppm 0.1. Kwa [[binadamu]] inaweza kukera [[pua]] na [[koo]] pamoja na kuleta [[kichefuchefu]]. Kuathiriwa kwa muda mrefu kunaweza kuleta kufura kwa [[mapafu]]<ref>[https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK208281/ Ozone backround information, Effects on humans], tovuti ya National Center for Biotechnology Information, iliangaliwa Mchi 2019</ref>.
 
Ppm 0.100 ni kiwango cha juu kinachoruhusiwa ndani ya karahana[[karakana]], [[viwanda]] au [[ofisi]] katika nchi kama [[Uingereza]], [[Japani]], [[Ufaransa]], [[Uholanzi]] na [[Ujerumani]].
 
==Matumizi==
Kutokana na nguvu yake ya kuoksidisha, ozoni hutumiwa kwa madhumuni mbalimbali:
 
* kusafisha [[maji]]: ozoni inaua [[bakteria]] na [[algae]] hivyo hutumiwa katika mchakato wa kusafisha maji kwa matumizi ya viwandani na maji ya kunywa
 
* kuua wajidudu[[wadudu]] katika utunzaji wa [[vyakula]] vilivyopikwa, pia kutunza [[nafaka]]
 
* [[uzalishaji]] wa [[madawa]]: ozoni hutumiwa katika michakato ya [[Kemia|kikemia kutokana na uwezo wake wa kuoksidisha]]
 
==Marejeo==
<references/>
{{mbegu-kemia}}
 
[[Jamii:Kemia]]