Tofauti kati ya marekesbisho "Bongo Flava"

no edit summary
'''Bongo Flava''' ni jina badala la [[muziki]] wa [[Hip hop ya Tanzania]]. Mtindo huu ulianzishwa kwenye [[miaka ya 1990]], hasa ukiwa kama mwigo au utokanaji wa [[hip hop]] kutoka [[Marekani]], ikiwa na ongezeko la athira ya muziki wa [[reggae]], [[rhythm and blues|R&B]], [[afrobeat]], [[dancehall]], na mitindo ya asili ya Kitanzania kama vile [[taarab]] na [[muziki wa dansi|dansi]], muunganiko ambao umeunda mtindo wa pekee wa muziki.<ref name="ReferenceA">Mueller, Gavin. "Bongoflava: The Primer." Stylus Magazine, 12 May 2005</ref> Mashairi kawaida huwa kwa lugha ya [[Kiswahili]] au [[Kiingereza]].
 
Jina la "bongo flava" ni tokeo la matini yaliyoharibiwa kutoka "bongo flavour", ambapo "bongo" ni wingi wa neno ''[[wikt:ubongo|ubongo]]'', ambapo mara nyingi huchukua nafasi ya kutaja jina la utani la [[Dar es Salaam]], jiji ambalo mtindo aina ya mtindo huu inatokea na wakati mwingine humaanisha pia nchi ya Tanzania. Katika bongo flava, sitiari ya "bongo" inaweza kutaja zaidi maana ya ujanjaujanja wa mtaani, ya ''msela'' au masela wingi wake.<ref>{{cite journal|last=Stroeken|first=Koen|title=Immunizing Strategies: Hip-Hop and Critique in Tanzania|journal=[[Africa (journal)|Africa]]|volume=75|issue=4|pages=488–509|date=Winter 2005|doi=10.3366/afr.2005.75.4.488}}</ref>
 
Istilahi ya "bongo flava" ilitajwa kwa mara ya kwanza mnamo 1996 na Radio One 99.6 FM (moja kati ya redio za kwanza kabisa za binafsi nchini Tanzania) DR wa Redio [[Mike Mhagama]] ambaye alikuwa akijaribu kutofautisha kati ya muziki wa R & B na hip hop wa Marekani kupitia lipindi chake maarufu cha redio - 'DJ Show' ambapo enzi hizo vijana chipukizi walikuwa hawajaanza kutamba kwa mitindo yao wenyewe. DJ Show kilikuwa kipindi cha kwanza cha redio kukubali wanamuziki vijana wa Kitanzania wenye athira ya muziki wa Marekani - wakijieleza wenyewe kupitia uimbaji wa rap. Alisema hewani, "Baada ya kusikiliza kibao cha "R & B Flava" kilichoitwa 'No Diggity' kutoka Marekani, sasa inakuja "Bongo Flava" kutoka kwa [[Unique Sisters]], kutoka hapa nyumbani." Baada ya kusema hivyo katika kipindi, istilahi hii ya "Bongo Flava" ikanasa hadi leo hii.