Maafa asilia : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
Mstari 58:
Dunia yetu inatembea katika [[anga-nje]] ikizunguka Jua letu. Hapa inakutana mara kwa mara na violwa vinavyoanguka kwenye [[angahewa]] na kuonekana kama [[vimondo]]. Vingi ni vidogo havileti hasara.
 
Lakini kama ni kiolwa kikubwa kama [[asteroidi]] inayogongakinachogonga Dunia hatari ni kubwa. Migongano hii hutokea mara chache sana lakini sayansi imetambua ya kwamba pigo la asteroidi kubwa miaka milioni 66 iliyopita lilisababisha kuangamizwa kwa spishi nyingi pamoja na [[dinosauri]]. Pigo hili lilirusha kiasi kikubwa cha vumbi kwenye angahewa pamoja na kusababisha milipuko ya volkeno nyingi na kuleta mabadiliko ya [[tabianchi]] kwa miaka kadhaa, hivyo kushusha halijoto duniani na kusababisha giza kwa muda mrefu.
 
Katika karne iliyopita kulikuwa na matukio mawili yaliyoonyesha nguvu haribifu ya violwa kutoka anga-nje:
*mwaka 1908 kimondo kikubwa au asteroidi ndogo iligonga eneo la [[Tunguska]] huko Urusi na kuangamiza kilomita za mraba 2,000 za misitu, Kwa bahati nzuri wakati ule hapakuwa na watu katika eneo la Tunguska.
* Mwaka 2013 kimondo kilichokadiriwa kuwa na kipenyo cha mita 17 pekee kilisababisha uharibifu kwa kulipuka juu ya mji wa [[Chelyabinsk]] nchini Urusi. Watu 1,500 walijeruhiwa, hasa na kioo cha madirisha kilichopasuka kote mjini wakati wa mlipuko. Nyumba nyingi zhiliathiriwaziliathiriwa.
 
Kutambuliwa kwa hatari hii imesababisha mataifa mbalimbali kushirikiana katika mipango ya kutambua mapema [[Kiolwa cha kukaribia dunia|violwa vinavyokaribia Dunia]].