Kasoko : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
[[Kasoko]] ([[ing.]] ''crater'') ni shimotundu kwenye ardhi kutokana na mlipuko au mshtuko wa kugongwa na gimba.
 
Kasoko ina umbo la duara; katikati ni kama shimo na ukingo wake unainuliwa juu ya uwiano wa mazingira yake. Duniani kasoko zinapatikana mara nyingi kutokana na milipuko wa volkeno au milipuko mingine. Kwenye sayari au miezi yenye uso thabiti kuna kasoko nyingi kama matokeo ya kugongwa na magimba kutoka anga-nje. Kwa mfano kwenye [[Mwezi wa Dunia]] kuna kasoko nyingi zilizosababishwa na migongano ya [[asteroidi]]. Pigo la kitu kigumu linarusha mata iliyopo mahali pa mgongano ikipangwa pembeni ya tundu hili kwa umbo la ukingo wa mviringo.
 
Duniani kasoko zilizosababishwa na mishtuko ya aina hii husawazishwa baada ya muda fulani kutokana na [[mmomonyoko]] wa mvua na upepo; kwenye magimba pasipo na angahewa kama Mwezini zinabaki kwa muda mrefu.
 
Kuna aina mbalimbali za kasoko
Line 9 ⟶ 13:
Kasoko kubwa zaidi duniani zilisababishwa na [[asteroidi]] zilizogonga Dunia yetu. Kasoko kubwa iliyojulikana hadi 2006 ilikuwa kasoko ya [[Vredefort]] nchini ([[Afrika Kusini]]) yenye umbo la yai ya urefu wa 320 km na upana wa 180 km.
 
Mwaka 2006 wataalamu waligundua kasoko kubwa zaidi yenye kipenyo cha 500 km huko [[Antarktika]] katika picha zilizopigwa kutoka angani. Iko chini ya barafu ya Antarktika katika eneo la Wilkes Land inatajwa kwa kifupi cha WLIC (kiinging.: Wilkes Land impact crater). Kasoko ya WLIC inaaminiwa imesababishwa na [[asteroidi]] yenye kipenyo cha takriban 5 km.
 
<gallery>
Line 17 ⟶ 21:
</gallery>
 
{{maana}}
 
[[Jamii:Jiografia]]
[[jamii:Astronomia]]