Jabuha Asadi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
 
Mstari 24:
==Jina==
Jabuha Asadi inayomaanisha “Paji la Simba” ilijulikana kwa mabaharia Waswahili tangu miaka mingi wakifuata njia yao baharini wakati wa usiku kwa msaada wa nyota. <ref>ling. Knappert 1993</ref>. Walipokea jina hili kutoka kwa Waarabu wanaosema kwa kawaida <big> جبهه الاسد </big> ''jabha al-asad'' inayomaanisha „paji la simba ". Jina hili limejadiliwa mara nyingi kwa sababu katika picha zote za kundinyota hii si sehemu ya kichwa zaidi la nywele za shingoni lakini unajimu wa Waarabu unajua « manzili za mwezi » na mojawapo ni « al jabha » inayojumlisha nyota kadhaa za Asadi (Simba) kwa hiyo inawezekana jina lilitokea hapa <ref>Allen (1899). uk. 259</ref>.
Kwa matumizi ya kimataifa [[Umoja wa Kimataifa wa Astronomia]] ulikubali jina la Kiarabu na kuorodhesha nyota ya γ1 kwa jina la "Algieba" <ref>[https://www.iau.org/public/themes/naming_stars/ Naming Stars], tovuti ya [[Umoja wa Kimataifa wa Astronomia]] (Ukia), iliangaliwa Novemba 2017</ref> . Hivyo sehemu nyingine ya nyota pachamaradufu γ2 haina jina.
 
Gamma Leonis ni [[jina la Bayer]] ingawa [[Gamma]] ni herufi ya tatu katika [[Alfabeti ya Kigiriki]] na Jabuha Asadi ni nyota angavu ya pili katika Asadi (pia: Simba) - Leo.
 
==Tabia==
Jabuha Asadi inatambuliwa kuwa nyota pachamaradufu kwa kutumia darubini ndogo.
 
Nyota kuu ina mwangaza unaoonekaka wa +2.28 ikiwa katika kundi la spektra K1-III. Jotoridi usoni ni K 4,470 na mng’aro wake kwenye Lo 180. Nyota ya B huwa na mwagaza unaoonekana wa mag +3.51 iko katika kundi la G7 III. Zinazungukana kwa umbali wa vizio astronomia 170 katika muda wa miaka 500 au zaidi. Zote mbili zimeshakwisha kuyeyunganisha hidrojeni kuwa heliamu zikapanuka katika hatua iliyofuata.