Mwangaza halisi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1:
'''Mwangaza halisi''' (kwa [[Kiingereza]] ''absolute magnitude'') ni [[kipimo]] cha ukali wa [[nuru]] ya [[nyota]] au [[gimba la angani|magimba mengine ya anga]] jinsi itakavyoonekana kwa mtazamaji aliye kwa umbali sanifu wa miakanuru 32.6 au [[parsek]] 10.
 
Mwangaza halisi ni tofauti na [[mwangaza unaoonekana]] jinsi tunavyoona nyota kutoka [[Dunia]]. Maana mwangaza tunaoona unategemea na ukubwa wa nyota, umbali wake na mambo mengine. Nyota ndogo na hafifu iliyo karibu nasi katika [[anga la nje|anga-nje]] itaonekana angavu kuliko nyota kubwa iliyo mbali. Hii ni sawa na kuangalia [[taa]] iliyo karibu au mbali.
 
Kipimo hiki kwa kutumia umbali sanifu kinawaruhusu [[wanaastronomia]] kulinganisha uang'avu wa magimba.