Nyota nova : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 11:
*Nova ya Tycho Brahe pamoja na ile ya mwaka 1006 siku hizi zinaitwa "[[supanova]]" maana zilikuwa ni milipuko ya nyota zilizoharibiwa wakati wa matukio haya. Inayobaki ni wingu la mata yake iliyosambaa katika eneo kubwa kama ile ya Nebula ya Kaa. Nishati inayopatikana katika mlipuko wa supanova inazidi ile ya kuwaka kwa nova mara nyingi, hivyo uteuzi wa jina la "supa"-nova (yaani nova kuu).
 
*Neno "nova" linafahamika sasa ni kuwaka kwa muda kwa nyota ndani ya [[nyota pacha|mfumo wa nyota pachamaradufu]]. Katika hali ya nova, nyota huongeza mwangaza ghafla mara elfu kadhaa ya kawaida yake hadi kurudi tena baada ya wiki au miezi katika hali yake kama kabla ya kuwaka. Pia hapa inawezekana kwamba wingu linabaki lakini nyota yenyewe bado iko.
 
==Tabia za nova==
[[Picha:Making a Nova.jpg|300px|thumb|Nyota Kibete Cheupe inavuta mata kutoka Jitu Jekundu jirani kwake.]]
Nyota nova za kawaida zinatokea katika [[Nyota pacha|mfumo wa nyota pachamaradufu]]. Nadharia inayokubalika na wengi inasema: [[nyota kibete cheupe]] na nyota kubwa, hasa [[jitu jekundu]], zinazungukana kwa umbali wa karibu. Kibete cheupe kimeshamaliza [[hidrojeni]] yake na kujikaza, hivyo [[graviti]] yake bado ni kubwa ingawa mjao wake ni mdogo, pia ina joto. Jitu jekundu la jirani linaendelea kupanuka. Hapa sehemu ya mata ya tabaka za nje ya nyota kubwa inavutwa na graviti ya nyota ndogo na kuhamia upande wake. Sehemu ya mata hii ni hidrojeni inayokusanyika kwa umbo la [[diski ya uongezekaji]]<ref>ing. "accretion disk"</ref> inayozunguka Kibete Cheupe na hatimaye kufikia karibu zaidi na kuunda angahewa. Hidrojeni hii inapashwa moto na uso wa Kibete Cheupe hadi kufikia halijoto ya kutosha ya kuanzisha [[myeyungano wa kinyuklia]] ''(nuclear fusion)''.
 
Mchakato huu unazalisha kiasi kikubwa cha nishati na kurusha sehemu ya hidrojeni inayowaka kwenye anga ya nje. Hii inaongeza mwangaza wa nyota inayoonekana sasa kama nyota nova. Kiasi cha masi inayorushwa angani wakati wa kuwaka inalingana takriban na <sup>1</sup>/<sub>10,000</sub> ya [[masi ya Jua]].