Kasoko ya dharuba : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 3:
'''Kasoko ya dharuba''' (kwa [[Kiingereza]] ''impact crater'') ni uwazi kwenye [[ardhi]] unaotokana na mshtuko wa kugongwa na [[gimba]]. [[Kasoko]] ina [[umbo]] la [[duara]]; katikati ni kama [[shimo]] na ukingo wake unainuka juu ya uwiano wa [[mazingira]] yake. [[Duniani]] kasoko zinapatikana mara nyingi kutokana na [[Mlipuko wa volkeno|milipuko]] ya [[volkeno]] au milipuko mingine.
 
Katika [[magimba ya angani]] yenye uso thabiti kuna kasoko nyingi kama matokeo ya kugongwa na magimba kutoka [[anga la nje|anga-nje]]. Kwa mfano, kwenye [[Mwezi (gimba la angani)|Mwezi]] wa [[Dunia]] kuna kasoko nyingi zilizosababishwa na migongano ya [[asteroidi]] au [[kimondo|vimondo]]. Pigo la [[kitu]] kigumu linarusha [[mata]] iliyopo mahali pa mgongano ikae pembeni kwa shimo hilo kwa umbo la ukingo wa [[mviringo]].
 
Duniani kasoko nyingi kutokana na mishtuko ya aina hiyo zinasawazishwa baada ya muda fulani kutokana na [[mmomonyoko]] unaosababishwa na [[mvua]] na [[upepo]]; kwenye magimba pasipo [[angahewa]] kama Mwezini zinabaki kwa miaka [[milioni]] kadhaa.