Jumamosi : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
d Protected "Jumamosi" ([Kuhariri=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho) [Kuhamisha=Zuia watumiaji wapya au wale ambao hawajajisajilisha] (bila mwisho))
 
Mstari 9:
 
== Jina la siku kwa Kiswahili na kwa lugha mbalimbali ==
Katika lugha ya [[Kiswahili]] jina la siku lina namba "1mosi" (moja) ndani yake. Hii ni dokezo la asili ya Kiswahili katika utamaduni yawa Kiislamu pasipo na athira ya [[Uyahudi]]. Hesabu inaanza baada ya sikukuu ya Kiislamu ya [[Ijumaa]] ambayo ni siku ya sala ya pamoja: [[Jumamosi]] kuwa siku ya kwanza baada ya Ijumaa, [[Jumapili]] kama siku ya pili, [[Jumatatu]] kama siku ya tatu n.k.. Tabia hii katika Kiswahili ni ya pekee hasa kwa sababu [[Kiarabu]] ambacho ni lugha ya [[Korani]] takatifu na lugha ya kimataifa ya Waislamu kinatumia jina la Kiyahudi na kuiita siku ya '''سبت''' (sabat) yaani [[Sabato]].
 
Lugha nyingi za nchi za Kiislamu zafuata kawaida ya Kiarabu na kuiita vilevile "Sabato" kwa mfano [[Kiindonesia]] (Sabtu) au [[Kiajemi]] (Farsi) (شنبه - shanbe, kutoka "shabat").
 
Katika lugha kadhaa za Ulaya jina la siku hutunza kumbukumbu ya mungu aliyeabudiwa zamani za dini ya Kiroma kama vile [[Kiholanzi]] "Zaterdag" au [[Kiingereza]] "Saturday" (yote: siku ya [[Saturnus]]). Lakini lugha zaidi za Ulaya hutumia pia jina la Sabato kwa namna mbalimbali kwa mfano [[Kifaransa]] "samedi" (kutoka [[Kilatini]] sambati dies - ''siku ya Sabato''), [[Kihispania]] "Sábado", [[Kirusi]] Суббота (subbota - ''pia Sabato'').
 
{{Siku za juma}}