Kalenga : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 9:
Kalenga ilikuwa [[makao makuu]] ya [[Mtemi]] [[Mkwawa]]<ref>[http://www.mkwawa.com/kalenga Fungu "Kalenga" kwenye Mkwawa.com], iliangaliwa Machi 2017</ref> aliyeongoza [[upinzani]] wa [[Wahehe]] dhidi ya [[Afrika ya Mashariki ya Kijerumani|ukoloni wa Kijerumani]] katika miaka ya [[1891]] - [[1896]].
 
Huko Kalenga Mkwawa aliwahi kujenga [[boma]] imara ya [[mawe]] baada ya kujifunza kuhusu uenezi wa Wajerumani kutoka sehemu za [[pwani]]. Boma hii liliitwa Lipuli. [[Ujenzi]] ulianza mnamo [[1887]] ukachukua miaka minne. Mji wote ulijulikana kama "Iringa" maana jina hili linataja mahali palipozungukwa na [[ukuta]]<ref>Glauning (1898) uk. 47; Glauning (aliyekuwa afisa wa jeshi la Kijerumani alitaja pia miji mingine iliyoitwa "Iringa" kama ilizungukwa na ukuta, kwa mfano Utengule wa Mtemi Merere wa Usangu</ref>.Kalenga-Iringa ilikuwa na sehemu mbili zilizotengwa na mto; upande wa kulia wa mto uliitwa "Unguja", upande wa kushoto "Bagamoyo". Mwaka 1891 kila sehemu ilikuwwa na msimamizi wake walioitwa Ngozingozi na Mtemiuma, waliuawa kwenye mapigano wa [[Lugalo]]<ref>[Nigmann (1908), uk 16-17]</ref>.
 
Baada ya kushindwa kwa [[jeshi]] la Kijerumani la [[Schutztruppe]] katika mapigano ya [[Lugalo]] mwaka 1891, Wajerumani walirudi kwa nguvu zaidi wakashambulia Lipuli - Kalenga kwenye [[Oktoba]] [[1894]] kwa [[silaha]] kali kama [[mizinga]] na [[bombomu]].