Milima ya Udzungwa : Tofauti kati ya masahihisho

Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 2:
'''Milima ya Udzungwa''' ni [[jina]] la [[Hifadhi ya mazingira|hifadhi]] inayopatikana katika [[bara]] la [[Afrika]], [[nchini]] [[Tanzania]], [[mkoa wa Iringa|mkoani Iringa]] karibu na mpaka wa [[mkoa wa Morogoro]], [[wilaya ya Kilombero]].
 
Hifadhi iko [[umbali]] wa [[kilometa]] 350 [[kusini]] mwa [[Dar es Salaam]], kilometa 65 kutoka katika [[Hifadhi ya Mikumi]].
 
Jina la hifadhi limetokana na [[milima]] hiyo ya Udzungwa (yaani nchi ya [[Wadzungwa]], [[tawi]] la [[Wahehe]]). [[Kilele]] cha juu ni [[Mlima Luhombero (Iringa)]] ([[mita]] 2,579).
 
Ina ukubwa wa [[kilometa mraba]] 1990, na ni hifadhi yenye [[hazina]] ya aina nyingi za [[mimea]], [[Ndege (mnyama)|ndege]] na [[wanyama]] ambao hawapatikani katika sehemu nyingine yoyote [[duniani]].
 
Kati ya aina kumi na moja za jamii ya [[nyani]] wanaopatikana katika hifadhi hii, mbili hupatikana katika hifadhi hii pekee ambao ni: "[[Mbega Mwekundu]] wa Iringa" (Iringa red colobus monkey) na "Sanje Crested mangabey" ambaye alikuwa hajulikani mpaka mwaka [[1979]]. Kuna aina nyingine nne za ndege ambao hawakufanyiwa uchunguzi ambao ni: [[chozi bawa jekundu]] (rufous-winged sunbrid) na jamii mpya iliyogunduliwa ya aina ya [[kwale]] wa Udzungwa zinazofanya hifadhi hii kuwa ni moja ya makazi makuu na muhimu ya ndege pori barani [[Afrika]].
 
Wanyama wengine wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na [[simba]], [[chui]], [[nyati]] na [[tembo]].
 
"African violet" ni [[ua]] ambalo linapatikana ndani ya hifadhi hii katikati ya [[miti]] mirefu inayofikia [[mita]] 30.
 
Pia [[Mto Sanje]] ni kivutio kikubwa sana. [[Mto]] huu una [[maporomoko]] ya [[maji]] yenye [[urefu]] wa [[mita]] zipatazo 170 yakianguka kupitia msituni na kututa mithili ya mianzo ya [[ukungu]] [[bonde|bondeni]].
 
==Tazama pia==