Troia : Tofauti kati ya masahihisho

53 bytes added ,  miaka 4 iliyopita
no edit summary
No edit summary
No edit summary
[[Image:Plan Troy-Hisarlik-en.svg|thumb|320px|Awamu za kukua kwa Troia kufuatana na utafiti wa akiolojia]]
[[File:Homeric Greece-en.svg|thumb|320px|Ramani ya Ugiriki ya Kale zamani za Homer]]
'''Troia''' (kwa [[Kigiriki]]: Τροία, ''troia'', pia: Ίλιον, ''ilion''; kwa [[Kiingereza]]: ''Troy'')<ref>{{cite web|first=Charlton T.|last=Lewis|coauthors=Charles Short|title=Ilium|work=A Latin Dictionary|publisher=Tufts University: The Perseus Digital Library|url=http://www.perseus.tufts.edu/cgi-bin/ptext?layout.reflang=la;layout.refdoc=Perseus%3Atext%3A1999.04.0059;layout.reflookup=Ilium;layout.refcit=;doc=Perseus%3Atext%3A1999.04.0059%3Aentry%3D%2321459|accessdate=2008}}</ref> ulikuwa [[mji]] wa [[Asia Ndogo]] zamani za [[Ugiriki ya Kale]]. Inajulikana kutokana na [[Iliadi|utenzi wa Iliadi]] ambamo [[mshairi]] [[Homer]] alisimulia habari za [[Vita yavya Troia]].<ref>{{cite book|first=Jenny|last=March|title=The Penguin Book of Classical Myths|date=2008|isbn=978-0-141-02077-8|publisher=Penguin Books|page=294}}</ref>
 
Kwa [[karne]] nyingi mahali pa mji hapakujulikana ingawa watu wengi walijaribu kupakuta kwa sababu ya umaarufu wa utenzi huo uliokuwa na maana sana katika [[utamaduni]] wa [[Ulaya]]. Mnamo mwaka [[1868]] [[Mjerumani]] [[Heinrich Schliemann]] alianza kuchimba kwenye [[kilima]] cha [[Hisarlik]] kilichopo karibu na mji wa [[Çanakkale]] [[magharibi]] [[kaskazini]] mwa [[Uturuki]]. Alikuta mabaki ya [[Jengo|majengo]] na kuta kubwa na baada ya majadiliano marefu leo hii [[wataalamu]] hukubaliana hapa palikuwa mahali pa Troia ya Kale.
==Tanbihi==
<references/>
{{mbegu-jio-Uturuki}}
 
[[Jamii:Ugiriki ya Kale]]
[[Jamii:Urithi wa Dunia]]
[[Jamii:Historia ya Uturuki]]