Wakazi wa kwanza walikuwa [[wamonaki]] kutoka [[Ireland]].
<br />
Kati ya miaka [[1035]] na [[1814]] visiwa vilikuwa chini ya Norwei. Ndipo vilipotolewa kwa [[Denmark]].
Kufikia mwanzo wa mwaka [[1540]] visiwa vilikuwa vimejiunga na [[Matengenezo ya Kiprotestanti]].
Kuanzia [[mwaka]] [[1948]] ni jimbo la nje la [[ufalme]] wa Denmark lenye madaraka ya pekee ya kujitawala. Visiwa vinaendesha shughuli zao isipokuwa [[siasa]] ya nje, [[jeshi]] na mambo ya [[mahakama]] ni chini ya [[serikali kuu]]. Hali ya kisiasa ndani ya Denmark inalingana na [[Greenland]] ambayo pia ni jimbo la nje la Denmark linalojitawala kwa kiwango kikubwa.
Visiwa vya Faroe viliamua kutoingia katika [[Umoja wa Ulaya]] pamoja na Denmark. Kumbe vimeunda [[umoja wa forodha]] na Iceland.
==Watu==
[[Picha:Tinganes.jpg|thumb|right|250px|[[Nyumba]] za [[serikali]] mjini [[Torshavn]].]]